loader
Dstv Habarileo  Mobile
Magufuli kuzikwa  makaburi ya familia

Magufuli kuzikwa makaburi ya familia

MAZISHI ya Rais wa Awamu ya Tano, John Magufuli yamepangwa kufanyika kwenye makaburi ya familia yaliyopo mtaa wa Lubambangwe, nyumbani kwake wilayani Chato, mkoa wa Geita.

Hayo yalisemwa jana na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel wakati akizungumza na waandishi wa habari kuelezea ratiba pamoja na maandalizi ya kuupokea mwili wa Rais Magufuli.

Alisema kwa mwongozo uliopo, utaratibu wa mazishi utasimamiwa na viongozi wa kitaifa, timu ya itifaki na wanafamilia ambao ndiyo pekee watahusika kumpumzisha kiongozi huyo kwenye nyumba yake ya milele.

Alisema anafahamu kuna wananchi wengi ambao wanataka kushiriki shughuli hiyo ya mazishi ya mpendwa wao siku ya Ijumaa, lakini kutokana na mwongozo huo haitawezekana kila mtu kushiriki.

"Kiongozi wetu atalazwa kwenye maeneo ya nyumbani kwenye makaburi ya familia na  utaratibu na maandalizi yanaendelea kufanyika, tukio hili ni kubwa, niwasihi tu watakaopata kibali siku hiyo ya tarehe 25 (kesho) na 26 (keshokutwa) ndiyo watashiriki," alisema Gabriel.

Mkuu huyo wa mkoa ametoa wito kwa wananchi mkoani hapa kujitokeza kwa wingi maeneo ya barabarani leo kuupokea na kuuaga mwili wa Rais Magufuli ambao utawasili mkoani hapa kutokea mkoani Mwanza.

Alisema uongozi wa mkoa wa Geita umejipanga kuupokea mwili wa kiongozi huyo kuanzia mpakani mwa Geita na Mwanza ambapo wananchi watakaojitokeza barabarani watakapewa fursa ya kuaga.

 

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi