loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tumwombee Samia ‘viatu’ vya Magufuli vimtoshe

Watanzania wapo katika maombolezo ya siku 21 kutokana na kifo cha Rais John Magufuli, Machi 17, 2021. Atazikwa kesho Chato mkoani Geita.

Aliyekuwa Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, aliapishwa Machi 19, 2021 kuwa Rais wa Tanzania akiwa mwanamke wa kwanza kuwa Rais nchini Tanzania. Tumwombee sana na tumsaidie kwa dhati.

Ninampongeza Samia kwa kuapishwa kuwa Rais wa Tanzania kwa kuwa kuapishwa kwake kumetokana na matakwa ya katiba, uchapakazi wake, uadili, umakini na msimamo ambayo ni mambo yaliyomfanya atumikie sawia katika kipindi cha kwanza cha miaka mitano walipoingia madarakani baada ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2015, na hata baada ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020.

Uchaguzi huo unaonesha wazi Rais Samia amefaa zaidi kuwa kiongozi na ndiyo maana amefikia hatua ya kuapishwa kuwa Kiongozi Mkuu (Rais) wa Tanzania.

Wakati tunaomboleza na kumuombea Mungu ampokee Magufuli na pia tukimpongeza Rais Samia, Watanzania tunawajibika kumwombea na kumsaidia ili viatu vya JPM alivyovaa Rais Samia, vimtoshe na ikibidi, ‘vimbane.’ Tumsaidie kwa hali na mali; kwa maneno na vitendo.

Miongoni mwa mambo tunayopaswa kumwombea na kumsaiddia, ni pamoja na afya njema, Mungu ampe moyo wa ujasiri na upendo zaidi kwa wanyonge wakiwamo maskini afuate nyayo za Magufuli kwa kuwa zaidi kiongozi wa kutumikia na si kutumikiwa.

Tumwombee na kumsaidia azidi kuuchukia umaskini kwa vitendo na tumsaidie kukataa ‘kubeba na kutembeza bakuri’ kwa mataifa ya nje kwa kuwa uwezo wa ‘kujaza bakuli kwa vyakula vyetu’ tunao maana Tanzania ni nchi yenye rutuba inayofaa kwa kilimo cha mazao mbalimbali, madini, bahari maziwa na mito; mbuga za wanyama na vivutio mbalimbali vya utalii na uwekezaji.

Viongozi waepuke tabia ya kutaka kutoa sifa ili kuziba udhaifu na uzembe wao, bali wafanye kazi yao ipasavyo. Wasisubiri rais awafanyie kazi. Tuwakate wwenye siasa za majitaka, wanaoweza kuyumbnisha nchi wakipewa nafasi ya ‘kusikika’ kila wanachosema.

Tumsaidie Rais wetu ili ‘vibaka’ wa uchumi wa Tanzania, wasitoroshe madini na wasaliti katu, wasiijaribu nchi. Tumwombee asimame imara kutetea wanyonge kama alivyoanza..

Tumsaidie Rais ‘kufunga milango’ yote ya ufisadi na utoroshaji wa rasilimali za nchi na kupambana kwa dhati dhidi ya uzembe kazini na hata vitendo vya rushwa na ufisadi kwa kuwa ni mambo yanayoweza kulitesa taifa.

Tuungane kumsaidia Rais ili majaribio ya kutaka kuirudisha nchi katika ukoloni wa kimatibabu, kiuchumi, kisiasa, wala kiulinzi na kiutamaduni, yashindwe na kufia mbali.

Wakati tunamsaidia, tumwombee Rais Samia avae viatu vya Magufuli kwa ‘kuwatumbua’ viongozi au watendaji wazembe, wabadhirifu na wanaiojaribu kulihujumu taifa.

Tumsaidie Samia aongoze Tanzania kama alivyofanya Hayati Magufuli na ikibidi, azidishe ubora ili watu mataifa yanayotuita maskini wajue tunawashangaa huku tukijiuliza: “Kama sisi ni maskini, mbona wanakuja kwetu?”

WATU hutegemea mvua ili kufanikisha shughuli mbalimbali, ikiwamo ...

foto
Mwandishi: Joseph Sabinus

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi