loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

CCM: Tutamuenzi JP kwa mengi

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) katika Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma, kimesema kitaendelea kumlilia, kumkumbuka na kumuenzi Rais wa Awamu ya Tano, Hayati John Magufuli kutokana na serikali yake kutekeleza miradi mikubwa ya maendeleo iliyobadili maisha ya wananchi.

Miongoni mwa miradi iliyotekelezwa katika Wilaya ya Songea ni ujenzi wa miundombinu ya barabara za lami katika mitaa mbalimbali, miradi ya maji, umeme, vituo vya afya, ujenzi wa shule za msingi na sekondari na ujenzi wa Kituo Kipya cha Mabasi cha Shule ya Tanga.

Hayo yalisemwa na Mwenyekiti wa CCM wilayani Songea, Hamis Abdallah Ali, wakati akizungumza na HabariLEO mintarafu chama, baada ya kifo cha Rais Magufuli aliyekuwa Mwenyekiti wa kitaifa wa chama hicho.

Alisema, CCM na wananchi wilayani Songea wamepokea kifo cha kiongozi huyo kwa masikitiko makubwa kwa kuwa wananchi walikuwa bado wanampenda wakiwa na matumiani tele ya maendeleo hasa wakizingatia kuwapo baadhi ya miradi aliyoahidi, lakini haijaanza kutekelezwa.

Alisema kuondoka kwake hapa duniani ni kama fumbo kubwa kwa Wanasongea ambao bado walitamani kumuona akimaliza kipindi chake cha miaka kumi kwa mafanikio makubwa, huku akiendelea na ujenzi wa miradi iliyoanza kujengwa chini ya uongozi wake na ile iliyopo kwenye ilani ya chama hicho.

Ali alisema taifa limempoteza kiongozi mpambanaji, shujaa na mwenye upendo kwa nchi yake.

 Aliwataka Watanzania kuendelea kudumisha amani, umoja, mshikamano na upendo uliokuwepo tangu enzi za waasisi wa taifa.

Aidha, Ali aliwaomba Watanzania kuendelea  kuomba Mungu ili ampe nguvu Rais wa sasa wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na kuiombe nchi ipate viongozi wazuri zaidi katika ngazi nyingine mbalimbali ambao  ni wachapakazi na waadilifu ili wamsaidia ipasavyo Rais Samia kutekeleza majukumu yake.

 

 

WATU hutegemea mvua ili kufanikisha shughuli mbalimbali, ikiwamo ...

foto
Mwandishi: Muhidin Amri, Songea

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi