loader
Dstv Habarileo  Mobile
RC Gabriel: Tumejiandaa kuishi bila Magufuli

RC Gabriel: Tumejiandaa kuishi bila Magufuli

MKUU wa Mkoa wa Geita, Robert Gabriel amesema wananchi mkoani humo wamejiandaa kuishi maisha mapya bila Rais John Magufuli.

Aliyasema hayo jana katika Uwanja wa Magufuli, Chato wakati viongozi na maelfu ya wananchi wakijiandaa kuuaga mwili wa Rais Magufuli na akabainisha kuwa, wataishi maisha yenye mwelekeo na maono aliyowaachia.

“Sisi tunamshukuru Mungu kwa kumuambia Mungu asante kwa zawadi ya maisha ya mzalendo namba moja wa Afrika kupitia Mkoa wa Geita ambaye leo hii tunapokwenda kumuaga, mbegu hii itakwenda kuzaa Magufuli wengi katika taifa hili,” alisema Gabriel.

Alisema, Rais Magufuli alikuwa mwadilifu, mfuatiliaji aliyetaka matokeo, aliyeleta heshima kwa Mwafrika na heshima kwa wanyonge wakiwemo masikini na watu wa makundi maalumu.

Alisema, Magufuli alitoa maisha yake katika kuwatumikia Watanzania na hakuwa na muda wa kukaa na familia yake na kwa kipindi kifupi aliishi kazi na wito wake.

“Tunaamini maisha haya yataleta mapinduzi kwetu kwa ambao ametuachia urithi huu mkubwa sana,” alisema Gabriel.

Alisema wameona mapinduzi ya Rais Magufuli katika kila eneo ikiwemo miradi ya maji, elimu, afya, madini yakiwemo masoko ya rasilimali hiyo adimu, ujasiriamali, na makundi maalumu na kwamba amefanya mema mengi na makubwa.

“Kama hukuona kazi kwenye uhai wake, kwa kifo chake nchi inaomboleza. Watanzania mmoja mmoja inaonyesha ni kwa namna gani maisha ya mtumishi huyu, kiongozi wetu mkuu Hayati Dk John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania yalivyokuwa ya kipekee,” alisema Gabriel.

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi