loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Asanteni - Rais Samia

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu amewashukuru watu wote walioshiriki mazishi ya Hayati Rais Dk John Pombe Magufuli kuanzia siku ya kifo chake mpaka hii leo ambapo mwili wake utazikwa katika makaburi ya familia yaliyopo Chato, Geita.

Akitoa shukrani zake Rais Samia amesema “Leo tunapompumzisha mpendwa wetu kwenye nyumba yake ya milele, kwa niaba yangu binafsi na niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, napenda kuwashukuru Watanzania wenzangu,”amesema Rais Samia.

Aidha, aliwapongeza viongozi wastaafu, viongozi wa nchi na mashirika mbalimbali ya kimataifa, viongozi wa dini na kisiasa, Jumuiya ya Kidiplomasia, vyombo vya habari, wasanii na kila wote walioshiriki.

“Tafadhali pokeeni shukrani zetu za dhati na muendelee kuiombea roho ya Hayati Dk Magufuli ipumzike kwa amani na Mungu aendelee kuifariji familia yake.” Aliongeza Rais Samia.

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi