loader
Sababu Kikwete kumpendekeza Magufuli urais

Sababu Kikwete kumpendekeza Magufuli urais

Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne, Jakaya Mrisho Kikwete amemsifu Hayati Rais Dk John Pombe Magufuli kuwa alikuwa miongoni mwa mawaziri waliojituma katika utawala wake na ndio sababu ya kupendekeza jina lake kwenye kinyang’anyiro cha urais mwaka 2015 na kuwa mgombee wa nafasi hiyo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).  

Kikwete ameyasema hayo leo wakati akitoa salamu za rambirambi katika Uwanja wa Magufuli uliopo Chato mkoani Geita, ambako viongozi mbalimbali akiwemo, Rais Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar, Hussein Mwinyi na wengine wamehudhuria ibada ya mazishi ya kuuaga mwili ya Hayati Rais Dk John Pombe Magufuli.

Akizungumza kwa kutaja yale aliyoshirikiana naye katika utawala wake, Kikwete alisema baada ya kuona juhudi zake katika wizara mbalimbali alichukua majina matano kati ya 38 la kwanza likiwa la hayati Magufuli na kuyafikisha mbele ya Kikao cha Kamati Kuu ambako kulikuwa na mjadala mkali na hatimaye jina la Magufuli kupitishwa.

“Wapo wazee wastaafu wakina mzee Mangula walinifuata na kuniambia vipi fulani usimuweke namwambia nimesikia, majina yale kwa mara ya kwanza niliyatoa kwenye kikao cha maadili ya  Chama Cha Mapinduzi, mjadala mkali kweli kwa  nini umemuacha fulani, hawa wepesi, hawatoshi,”alisema Kikwete.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/e47cad186be15f8a83f05a0d6b4c3c54.jpg

MWENGE wa Uhuru unaendelea ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi