loader
Samia: ‘Hapa Kazi Tu’ palepale

Samia: ‘Hapa Kazi Tu’ palepale

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema falsafa ya Hapa Kazi Tu itaendelea kufanyiwa kazi na ahadi zote zilizoko kwenye ilani na zile binafsi alizotoa Dk John Magufuli nchi nzima zitatekelezwa.

Rais Samia aliyasema hayo jana alipotoa salamu za pole kwa Watanzania katika shughuli ya mazishi na baadaye maziko ya hayati Rais Magufuli yaliyofanyika nyumbani kwake Chato mkoani Geita.

Alisema Watanzania wamempoteza jemedari wao lakini aliyoahidi yatatekelezwa kwa kuwa Dk Magufuli alikuwa mwalimu mzuri.

“Ule wasiwasi ulioelezwa moyoni kwamba Magufuli ameondoka... Kinachofuata ni kutekelezwa kwa ahadi zote zilizoko ndani ya ilani na ahadi alizotoa Magufuli kwa watu wake. Na hili si kwa watu wa Chato pekee bali kwa mikoa yote ya Tanzania.”

Samia alisisitiza, “Tunakwenda kumpuzisha baba, shujaa ninachotaka kuwaambia Watanzania Dk Magufuli ameitwa na Mungu na ameitika. Tunachokwenda kusitiri ni kiwiliwili lakini maono mikakati na falsafa yake hapa kazi itaendelea kuwapo na tutaendelea kuifanyia kazi.”

Aliwataka wote wanaotoa huduma kwa wananchi serikalini, binafsi na hata viongozi wa dini kuonesha ushirikiano, mshikamano na upendo kwa taifa. Alisema hiki ni kipindi ambacho panahitajika kuonesha upendo. “Tusiyumbe na tusiyumbishe taifa. Tukaendeleze taifa la Tanzania.”

“Ni mazito lakini ni ya Mungu naomba tupokee,” Alisema na kutoa pole kwa familia na watoto wa marehemu na kuwahakikishia kwamba msiba huo ni wa wote na kwamba serikali itakuwa nao, hatawaacha.

Alizungumzia ombi la kutaka Chato uwe mkoa, Samia alisema anazo taarifa kwamba mchakato umeanza. Aliagiza umalizike na wafikishe serikalini waangalie vigezo vigezo kama vimekidhi na endapo havikidhi, ielekeze cha kufanya. “Kwa ajili ya kumuenzi, naomba kamilisheni tuone jinsi tunaweza kufanya,” alisema Rais.

Kuhusu tatizo la upungufu wa dawa kama ilivyoelezwa katika salamu za wazee wa Chato, Rais alisema amebeba suala hilo na kwenda kufanyia kazi akitambua kwamba katika miaka mitano serikali iliondoa upungufu mkubwa wa dawa. Hata hivyo aliahidi kulifanyia kazi na kwamba dawa zitapatikana.

Rais Samia alishukuru kamati iliyoshughulikia msiba huo, vyombo vya ulinzi na usalama na familia na ofisi binafsi ya Magufuli kwa kazi kubwa waliyofanya kuanzia kwenye kuuguza hadi kumzika.

Aliungana na Spika wa Bunge, Job Ndugai kunukuu kitabu cha Isaya 41 katika Biblia akisisitiza kwamba taifa limeondokewa lakini Mungu hataiacha nchi. “Tuendelee kumwelekea Mungu naye atatushika mkono tuende vile tulivyojipanga,” alisema.

Aliendelea, “Tunakwenda kumpuzisha baba, shujaa ninachotaka kuwaambia watanzania dk magufuli ameitwa na Mungu na ameitika. Tunachokwenda kusitiri ni kiwiliwili lakini maono mikakati na falsafa yake hapa kazi itaendelea kuwapo na tutaendelea kuifanyia kazi.”

Aliwataka wote wanaotoa huduma kwa wananchi serikalini, binafsi na hata viongozi wa dini kuonesha ushirikiano, mshikanmano na upendo kwa taifa. Alisema hiki ni kipindi ambacho panahitajika kuonesha upendo. “Tusiyumbe na tusiyumbishe taifa. Tukaendeleze taifa la Tanzania.”

Akieleza masikitiko yake kwa kifo cha Dk Magufuli, Samia alisema alifika Chato mara mbili; wakati wa kampeni za urais mwaka 2015 kunadi sera na Ilani ya CCM na kumfariji Dk Magufuli alipofiwa na dada yake. Alisema alitegemea angefika tena Chato ili ampokee lakini badala yake amekuja kuhitimisha safari ya kaka, mlezi na mwalimu hapa duniani.

Alitumia fursa hiyo kuwashukuru viongozi wa dini kwa namna wanavyounga mkono Serikali wakati wote na wageni kutoka nje ya nchi waliofika Dodoma kushiriki mazishi ya kitaifa, Dodoma. Samia alimshukuru Mungu kwa kufika siku ya jana ya kumsitiri Dk Magufuli na kushukuru pia kamati na watu wote waliofanikisha shughuli nzima ya mazishi na maziko ya jana.

Awali akimkaribisha Rais Samia, Mkuu, Kassim Majaliwa na Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi ya Kitaifa alisema madaktari wanaendelea kumhudumia mama wa aliyekuwa Rais wa Tanzania, Dk John Magufuli, Suzana Ngolo Mussa mpaka afya yake itengamae.

Majaliwa alisema Rais Samia alimuagiza ahakikishe madaktari wanaomuhudumia mama huyo na wanaendelea kufanya hivyo mpaka afya itakaporejea.

"Najua leo tuko hapa kwa ajili ya mpendwa wetu Dk Magufuli kumpumzisha katika nyumba yake ya milele lakini tukumbuke kuwa mama yake yupo kitandani amelala, niseme nimetekeleza hilo na madaktari watamuhudumia mpaka afya yake itengemae," alisema Majaliwa.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/32baeb8f3f0ecaa183b02e753a8dbd39.jpeg

MKUU wa Mkoa wa Geita, ...

foto
Mwandishi: Gloria Tesha, Chato

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi