loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Makocha waishauri Stars

TIMU ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imeshindwa kufuzu fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) baada ya kichapo cha bao 1-0 walichopata kwa Guinea ya Ikweta katika mchezo uliochezwa juzi ugenini.

Stars ilikuwa inahitaji sare au ushindi ili kujiweka mguu mmoja ndani, lakini kupoteza mchezo huo kumewapa nafasi Guinea ya Ikweta kuifuata Tunisia kufuzu baada ya kufikisha pointi tisa ambazo Tanzania hata kama itashinda kesho dhidi ya Libya mchezo wa mwisho haiwezi kwenda popote.

Kufuatia matokeo hayo, baadhi ya makocha na wachambuzi wa soka wamezungumza na gazeti hili namna walivyoona na nini kifanyike, ambapo wamesema timu haikucheza kwa kiwango kama ilivyotarajiwa. Kocha Charles Mkwasa alisema timu haikucheza kwa kiwango kizuri pengine kutokana na walivyokuwa wameandaliwa.

“Wachezaji waliokuwepo wameshindwa kufanya kile kilichotarajiwa, wamecheza kiwango cha chini, walikuwa hawatengenezi mashambulizi, pengine mfumo waliotumia umeshindwa kuwasaidia,” alisema Kocha huyo wa zamani wa Stars na Yanga.

Mkwasa ambaye kwa sasa ni Kocha wa Ruvu Shooting alisema kinachohitajika sio kumlaumu kocha kwasababu bado ni mgeni bali kujipanga kwa ajili ya michuano ijayo kwa kuhakikisha timu inaanza kujengwa kuanzia sasa.

Kwa upande wake, mchambuzi Ally Mayai alisema ni majonzi kupoteza nafasi ya kufuzu kwani walitegemea kutokana na idadi ya timu kuongezwa katika michuano hiyo mikubwa labda Tanzania ingetumia fursa hiyo kucheza vizuri. Alisema timu ilikosea namna ilivyochukulia mchezo huo, mashambulizi yalikuwa hayafiki mbele na kuwapa nafasi zaidi wapinzani kuwashambulia kila mara.

“Tuliruhusu kushambuliwa zaidi na matokeo yake tukawa tunanyang’anywa mipira kirahisi na ukiwa unaruhusu mashambulizi lazima kuna muda utafanya makosa,”alisema.

Mayai alisema kinachohitajika ni kuwa na mkakati wa kujiandaa na Afcon ijayo na kwamba lazima kuwe na kundi la wachezaji wengi vijana wafike hata 100 ukiwa ni mpango wa muda mfupi wa kuandaa timu mapema.

Kwa upande wake, Kocha Msaidizi wa Tanzania Prisons, Shaban Kazumba alisema Kocha Mkuu hapaswi kulaumiwa kwani alipanga kikosi kwa kukariri wale aliowahi kufanya nao kazi huko nyuma.

Alisema saikolojia na maandalizi dhidi ya wapinzani yalichukuliwa ya kawaida lakini wapinzani walikuwa wako vizuri na walijiamini kwa vile walikuwa kwenye uwanja wao wa nyumbani. Kazumba alisema Kocha Kim Poulsen anahitaji apewe muda afuatilie wachezaji atapata timu anayotaka.

WASHINDI wa Michezo ya Mei Mosi wanatarajia kukabidhiwa zawadi zao ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi