loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

SHIMIWI KUMUENZI MAGUFULI KWA VITENDO

SHIRIKISHO la Michezo la Wizara na Idara za Serikali Tanzania (Shimiwi) limewataka wanachama wake kuendeleza yote yaliyokuwa yakisisitizwa na aliyekuwa Rais Dk John Magufuli katika michezo na kazi.

Hayo yalisemwa jana na Naibu Katibu Mkuu wa Shimiwi, Alex Temba alipozungumza kuhusu taasisi hiyo ya michezo itakavyomuenzi Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, 2021 Dar es Salaam.

Temba alisema kuwa Shimiwi na Watanzania wote wamepata pigo kubwa kwa kuondokewa na Dk Magufuri ambaye alikuwa mchapakazi hodari nchini na mtetezi wa wote, hasa wanyonge.

Alisema kuwa ili kumuenzi Dk Magufuli uongozi wa Shimiwi unawataka wanachama wake wote ambao zaidi ya 3,000 kufanya kazi kwa bidii kuendeleza michezo na nyanja zingine sehemu zao za kazi.

Alisema kwa kuwa wanachama wao wanatoka katika taasisi mbalimbali jukumu lao kubwa ni kuchapa kazi kwa bidii kama alivyokuwa akisema kila mara Dk Magufuli ili kuliinua taifa letu kiuchumi.

Alisema kuwa watakapokutana katika vikao vyao, ambavyo hushirikisha Shimiwi, Shimisemita, Shimuta na Bammata watajadili kwa kina jinsi ya kumuenzi rais huyo wa tano wa Tanzania.

Pia Temba alisema kuwa wanampa pole, na kumpongeza Samia Suluhu Hassan kwa kumpoteza Dk Magufuli na kuapishwa kuwa Rais wa Sita wa Tanzania wakiwa na matumaini makubwa kwake.

WASHINDI wa Michezo ya Mei Mosi wanatarajia kukabidhiwa zawadi zao ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi