loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kazumba tutaendelea tulipoishia

KOCHA Msaidizi wa timu ya Tanzania Prisons, Shaaban Kazumba ametamba kuwa amejizatiti kuhakikisha kikosi chake kinawasha moto na kupata matokeo mazuri na watahakikisha wanaendeleza walipoishia ili kusaka nafasi ya nne ambayo ndiyo malengo yao ya msimu huu.

Kazumba ana kaimu nafasi ya kocha Salum Mayanga ambaye yuko nje ya mchezo wa soka akiendelea na matibabu kutokana na kutetereka kiafya.

Akizungumza jana Kazumba, alisema kuwa wanatarajia kuingia kambini leo (jana)  kwaajili ya kuendelea na mazoezi ya kujiandaa na mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania dhidi ya Dodoma Jiji watakapokuwa nyumbani katika Uwanja wa Nelson Mandela mkoani Rukwa.

“Tumekuwa na muendelezo mzuri katika michezo minne mfululizo kabla ya mapumziko ya ligi naamini tutaendelea tulipoishia ili kujiwekea katika mazingira mazuri yakutimiza malengo yetu,” alisema.

Kazumba alisema kuwa anajua utakuwa mchezo mgumu kwa kila timu kwani Dodoma Jiji ni miongoni mwa timu zenye upinzani mkubwa msimu huu, lakini atatumia uwanja wa nyumbani kama silaha ya kupata pointi tatu, ambazo anazihitaji kwa udi na uvumba.

WASHINDI wa Michezo ya Mei Mosi wanatarajia kukabidhiwa zawadi zao ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi