loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Stars yasaka heshima 

TIMU ya Taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’ inatarajiwa kuikabili timu ya Libya katika mchezo wa kukamilisha ratiba  hatua ya makundi kufuzu fainali za mataifa ya Afrika ‘Afcon’ utakaochezwa saa 10:00 kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Stars imepoteza mchezo uliopita dhidi ya Equtorial Guinea kwa kufungwa bao 1-0, matokeo yaliyowaondoa katika harakati za kuwania nafasi ya kufuzu.

Waliofuzu Kundi J ni Tunisia yenye pointi 10 na Equtorial Guinea yenye pointi tisa ambazo hata kama Stars itashinda mchezo wa leo haiwezi kuwapeleka popote kwa kuwa watakuwa wamefikisha pointi saba ambazo ni chache kuliko walio juu yake.

Kadhalika kwa Libya nao pia, hata wakishinda hawaendi popote zaidi kwani nao wanakamilisha ratiba.

Licha ya kuwa hawana nafasi tena, Stars inahitaji ushindi utakaosaidia kuwaweka vizuri katika viwango vya soka ambavyo vimekuwa vikitolewa kila mwezi na Shirikisho la Soka Duniani (Fifa).

Stars na Libya walikutana katika mchezo wa kwanza ugenini ambao ulichezwa nchini Tunisia kutokana nchi hiyo kukabiliwa na machafuko ya vita na kushinda mabao 2-1.

Mchezo wa leo unaweza kuwa muhimu kwa Stars kushinda kwa ajili ya furaha ya mashabiki ambao wanapenda kuona burudani.

Pia, kuona nyota wao wanaocheza soka la kulipwa nje ya nchi kama Mbwana Samatta katika ligi ya Uturuki kwenye klabu ya Fernabahce, Simon Msuva anayecheza Wydad AC ya Morocco na wengine. 

WASHINDI wa Michezo ya Mei Mosi wanatarajia kukabidhiwa zawadi zao ...

foto
Mwandishi: Grace Mkojera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi