loader
Dstv Habarileo  Mobile
Kane hana hakika na hatima yake Tottenham

Kane hana hakika na hatima yake Tottenham

NYOTA wa Tottenham, Harry Kane amesema kwa sasa hajajua hatima yake katika klabu hiyo ya Ligi Kuu na kukanusha taarifa kwamba anaweza kuondoka msimu huu.

Kane, 27, amekuwa mchezaji tegemeo Spurs kwa sasa, shukran kwa mabao yake mengi kwa klabu hiyo.

Uwezo wake wa kufunga mabao umefanya klabu kubwa Ulaya kumfuatilia mshambuliaji huyo wa England.

“Nadhani hilo ni swali gumu kulijibu kwa sasa,”  Kane aliwaambia waandishi wa habari waliomuuliza kama ana mpango wa kuondoka Tottenham ili ashinde mataji kwingine.

“Muhimu kwa sasa ni kwamba nguvu zangu zote zipo kwenye mechi mbili za England na kumaliza msimu dhidi ya Spurs na baadae Euro.”

“Kufikiria kuhusu tetesi kunaweza kunivuruga hasa kiwango change. Mara zote napenda kuelekeza nguvu zangu kwenye jambo moja na hilo ni kumaliza vizuri na Spurs, kushinda mechi mechi zote za kufuzu na England na ninahakika tutakuwa mashindano mazuri ya Euro.”

“Tazama, najaribu kuwa mbali na tetesi kila iwezekanavyo, nimeelekeza nguvu zangu kwenye kufanya kazi yangu uwanjani kuanzia sasa mpaka mwisho wa msimu kisha tutaona wapi pa kwenda kutoka hapo.”

Kane alijiunga na Spurs akiwa na umri wa miaka 11 na kucheza soka yake kwa weledi kwenye klabu hiyo.

Mpaka sasa amefunga mabao 215 katika mechi 327 katika michuano yote akiwa nafasi ya pili kwenye mfungaji wa muda wote wa klabu hiyo nyuma ya Jimmy Greaves.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/88433515227db39300440e3cb5f58910.jpg

WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi