loader
Dstv Habarileo  Mobile
Shirika la Ndege Kenya  lapata hasara bilioni 36.2/-

Shirika la Ndege Kenya lapata hasara bilioni 36.2/-

SHIRIKA la Ndege Kenya liimepata hasara ya Sh bilioni 36.2 mwaka jana ambayo ni hasara kubwa katika historia ya shirika hilo.

Mapato ya shirika hilo yamepungua kwa takribani asilimia 60 hadi kufikia Sh bilioni 52.8, huku idadi ya abiria ikipungua kwa asilimia 65.7 hadi kufikia milioni 1.8 katika kipindi cha mwaka huo na kusababisha mapato kupungua kutoka Sh bilioni 103.6 mpaka Sh bilioni 33.7 kutokana na janga la covid -19.

Taarifa iliyotolewa na mwenyekiti wa shirika hilo, Michael Joseph ilisema mwaka jana duniani ulikuwa mwaka mbaya katika historia ya usafiri wa sekta ya anga.

Alisema kwa mara ya kwanza katika historia yake, shirika hilo lilisitisha shughuli zake kuanzia Aprili hadi Julai, 2020 kufuatia agizo la serikali la kusimamisha huduma zote za abiria zilizopangwa ndani na nje ya nchi ili kuzuia kuenea kwa covid-19.

"Baada ya kuanza tena kwa shughuli Agosti, mwaka jana, bado  mtandao wa biashara  ulishuka wakati athari za janga hilo zinaendelea kuonekana na vizuizi vya kusafiri vikiwa bado vimeenea katika maeneo mengine muhimu duniani,"  alisema Joseph.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/26446165087f12a1345dce615d3f600c.jpg

MAVUNO ya mahindi katika mwaka huu ...

foto
Mwandishi: NAIROBI

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi