loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mpango: Rais Samia nitume, niko tayari

MAKAMU wa Rais, Dk Philip Mpango amemwahidi Rais Samia Suluhu Hassan kwamba yupo tayari kuchapa kazi na yuko tayari kutumwa.

Akizungumza baada ya kuapishwa Ikulu, Chamwino mkoani Dodoma jana na Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma mbele ya Rais Samia, Dk Mpango alisema atakuwa msaidizi mwaminifu, mtiifu na mzalendo wa kweli kwa nchi yake.

“Sasa nipo tayari unitume kazi... Nitakuwa msaidizi mwaminifu na mtiifu na mzalendo wa kweli kwa nchi yangu,” alisema Dk Mpango ambaye kabla ya uteuzi wake juzi alikuwa Waziri wa Fedha na Mipango.

Aliahidi atakuwa mwaminifu, na hatakuwa kama Yuda Isikarioti aliyemsaliti Yesu kwa vipande 30 vya fedha.

“Kesho (leo) kwa Wakristo ni siku muhimu, siku ambayo Yuda Isikarioti alimsaliti Yesu Kristo kwa vipande 30 vya fedha. Sitakuwa kama huyo Yuda, sitakusaliti. Nitatekeleza kwa bidii na weledi kazi zote utakazonielekeza na majukumu yangu yote yaliyopo kwenye Katiba Ibara ya 47,”alisema Dk Mpango.

Alisema yupo tayari kuchapa kazi mchana na usiku na kuhakikisha ahadi zilizomo ndani ya Ilani ya CCM ya Mwaka 2020-2025, na maono ya Rais na kwa ajili ya ustawi wa wananchi, anavitekeleza kwa ufanisi. Alisema katika kutekelezamajukumu hayo na atakayotumwa na Rais, atashirikiana na viongozi wengine inavyopaswa wa pande zote mbili za za Muungano, pamoja na viongozi wa mihimili yote ya dola ikiwemo Bunge na Mahakama.

Alisema hakutegemea kupata nafasi hiyo, hivyo alisema hana maneno ya kumshukuru Rais Samia kwa uamuzi wake wa kumchagua kushika nafsi hiyo kubwa.Dk Mpango alimpongeza Rais Samia kwa kushika hatamu ya kuongoza taifa katika giza nene la msiba wa kuondokewa na Rais wa Awamu ya Tano, Dk John Magufuli, na akasema kwa sasa Watanzania hawana hofu tena na uongozi wake na wanaendelea kumuombea kuwa na afya njema na maisha marefu.

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, ...

foto
Mwandishi: Matern Kayera

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi