loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

…Samia amtaka amalize kero za Muungano

RAIS Samia Suluhu Hassan amesema amemchagua Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango kutokana na uchapakazi wake, weledi na utendaji wake, lakini hasa akakamilishe kutatua kero za Muungano.

Akizungumza baada ya kushuhudia kuapa kwake, Rais Samia alisema changamoto moja iliyokwama ilikuwa kuhusu fedha, hivyo amepewa Dk Mpango ili kutafuta wakamishwaji wengine ondoe changamoto hiyo.

Alisema kama alivyosema Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi alisema katika masuala ya Muuungano kazi ya uhusiano shughuli ya uhusiano ya kifedha kati ya Bara na Serikali ya Mapinduzi ni shughuli haikupata ufumbuzi.

Makamu wa Rais Mpango aliikalia yeye. “Mwanga mpe mtoto akulelee, sasa ni matumaini umetafuta wanga wenzio kulimaliza suala lililobaki ili kulimaza suala hilo,” Rais Samia alimuagiza Makamu wake.

Alisema mbali na majukumu ya kikatiba, Makamu wa Rais atamsaidia katika masuala ya kiuchumi, udhibiti fedha za serikali kwani ndiye mtu safi wa kwenda naye katika mjukumu hayo.

Rais Samia alisema alipendezwa na jina la Mpango anaamini ni mchapakazi na mwaminifu katika utendaji wake na amevutiwa pia na jina la Mpango kwani Philip ni mcha Mungu, mchumi mahiri, mchapakazi na mtendaji bora.

Kwa upande wake, Rais wa Zanzibar, Dk Mwinyi amemwahidi Makamu wa Rais kwamba atampa ushirikiano wote katika kufanya kazi zake hasa kutatua changamoto za Muungano.

Dk Mwinyi alisema ana imani kubwa atafanya kwa ufanisi katika utatuzi wa kero za Muungano zinazobaki na zinazoibuka. “Sina shaka chini ya uongozi wako zitamalizwa changamoto za Muungano zilizopo na mpya zitakazojitokeza,” alisema Dk Mwinyi.

Naye Spika wa Bunge, Job Ndugai alimpongeza Rais Samia kwa kumteua Dk Mpango kutoka miongoni mwa wabunge, na alimpongeza Dk Mpango kwa niaba ya wabunge kuaminiwa na kuteuliwa kushika nafasi hiyo.

Jaji Mkuu, Profesa Juma amewataka Watanzania kufanya kwa bidii na kuacha kupeleka matatizo madogo madogo wapeleke mambo makubwa ili kuwapa nafasi kufanya kazi nyingine viongozi hao.

“Tufanye kazi zetu, tusipeleke vitu vidogo vidogo, tupeleke kwao mambo makubwa tu,” alisema Profesa Juma na kuwataka Watanzania kufanya kazi kwa kufuata sheria na taratibu. Alisema sheria zinaweza kufanya mambo mazuri, lakini tatizo ni binadamu ambao wanaweza kuzitumia sheria vibaya na kusababisha matatizo.

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi