loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kaka wa Mpango, bosi CCM wajivunia uteuzi

KAKA wa Makamu wa Rais, Dk Philip Mpango, Dk Gerald Mpango amesema Rais Samia Suluhu Hassan amechagua mtu sahihi kwa wakati sahihi kumsaidia hivyo nchi itarajie maendeleo makubwa.

Amesema Dk Mpango ni mpole, lakini watu wakifanya mambo ya ovyo ni mkali na hana mchezo na rushwa.

“Ana uwezo mkubwa sana na Mheshimiwa Rais Samia (Suluhu Hassan) amechagua mtu mwenye uwezo atamsaidia sana kwa kazi zake, sana tu. Nashukuru wabunge wote wamemuunga mkono amepata asilimia 100 hawakukosea, wala Rais hakukosea na tutaona maajabu ya kazi zake,” alisema Dk Mpango wakati akizungumza kwenye kipindi cha Morning Express cha Kituo cha redio cha U FM cha Dar es Salaam.

Rais Samia alimteua Dk Mpango Machi 30, mwaka huu, siku hiyohiyo Bunge lilimthibitisha na Machi 31, mwaka huu Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma alimuapisha katika Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma.

Katibu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Kigoma, Kajoro Vyohoroka alisema mwaka jana Dk Mpango alipokwenda ofisini kwake wakati wa mchakato wa kugombea ubunge Jimbo la Buhigwe alimuomba ampeleke kwa viongozi wa dini.

“Toka achaguliwe kuwa mbunge amerudi mara tatu jimboni na jimbo lake lina kata ishirini Jimbo la Buhigwe, lakini ameshatembelea kata 12 mpaka leo kwenda kushukuru wananchi kwa kumchagua…sasa ni tofauti na wabunge wengine. Wengine mpaka leo hawajafanya mikutano ya kushukuru kwenye maeneo mengine,” alisema.

Mwenyekiti wa Chama Cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba alisema anaamini Dk Mpango atamsaidia Rais Samia na anashauri kiongozi huyo apewe jukumu la kuongoza Kamati Ndogo ya Uchumi ya Baraza la Mawaziri.

“Ni vema Rais Samia Suluhu Hassan akamtumia Makamu wake wa Rais kuweza kuandaa majukumu yanayopimika kwa kila waziri. Kwamba katika kila mwaka wa fedha kila Waziri katika wizara yake na makatibu wakuu wake wawe na mipango inayopimika,” alisema mchumi huyo maarufu nchini.

Makamu wa Mkuu wa Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam (UDSM), Profesa William Anangisye alisema Dk Mpango ni mtu wa vitendo na unaweza kuona uadilifu katika utendaji wake.

“Kwa hiyo, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa kweli kinajivunia sana katika hili ambalo limetokea la uteuzi wa Makamu wa Rais kwa awamu hii nyingine,” alisema.

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi