loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wanamichezo kuendelea kumkumbuka Dk Magufuli

RAIS wa tano wa Tanzania, Dk John Magufuli aliyefariki dunia Machi 17 na kuzikwa nyumbani kwake Chato mkoani Geita Machi 26, 2021, atakumbukwa daima na wanamichezo.

Magufuli alifariki kwa matatizo ya moyo katika hospitali ya Mzena, Dar es Salaam, kifo chake kilitangazwa hadharani na aliyekuwa Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan (ambaye sasa ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania).

Pumzika kwa amani Baba Magufuli baada ya kazi kubwa uliyofanya ya kulitumika taifa kwa miaka mitano na miezi kadhaa.

Magufuli amefanya mengi wakati wa uhai wake ikiwemo serikali yake aliyoingoza kugusa maeneo mbalimbalio ikiwemo michezo, ambayo kwa miaka mingi ilisahaulika.

Tunakumbuka jinsi Magufuli alivyosaidi mchezo wa soka pale alipotoa fedha kiasi cha Sh bilioni 1 kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kwa ajili ya kuandaa fainali za Mataifa ya Afrika zilizofanyika nchini mwaka 2019.

Fainali hizo za wachezaji wenye umri chini ya miaka 17 ziliandaliwa kwa ustadi mkubwa hadi TFF kupongezwa kwa kufanikisha mashindano hayo.

Magufuli pia aliwaita Ikulu wachezaji wa timu ya taifa, Taifa Stars, pamoja na viongozi wa soka nchini kuwapongeza baada ya kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika, Afcon 2019 Misri.

Tanzania kwa zaidi ya miaka 39 ilikuwa haijawahi kufuzu kwa Afcon tangu ilipocheza kwa mara ya mwisho mwaka 1980 Nigeria na ilipofuzu kwa fainali za 2019, Magufuli akawaita wachezaji Ikulu na kuwapongeza na kuwapa viwanja makao makuu ya nchi Dodoma.

Mbali na soka, Magufuli pia alisaidia michezo mingine kama ngumi, judo na mingine, ambayo huko nyuma ilishindwa hata kushiriki mashindano ya kimataifa kutokana na uhaba wa fedha.

Mfano katika ngumu za ridhaa alisaidia kupatikana kwa ulingo wa kuchezea ngumu wakati katika judo kwa sasa wanajiandaa kushiriki masindano ya kufuzu kwa Michezo ya Olimpiki, huku fedha wakipewa na Serikali.

Hakuna shaka kuwa wadau na wanamichezo nao watamkumbuka Magufuli kama zilivyo sekta zingine, ambazo zimefanyiwa mengi na mkuu huyo wa nchi, ambaye hakuwa na upendeleo.

Wanamichezo wataendelea kumkumbuka Rais Magufuli kwa mema aliyoifanyika nchi hii katika upande wa michezo na sehemu nyingine kwani wanamichzo nao mbali na kufaidika na mambo ya michezo, pia wanafaidi na mambo mengi yaliyoendelezwa na Magufuli.

Wanamichezo nao kama watu wengine wanafaidi miundo mbinu mbalimbali iliyotengenezwa na Magufuli na vitu vingine.

Yote na yote wadau wa michezo nao hawatamsahau Magufuli na kikubwa Mungu aiweke Roho yake mahali pema peponi. Amina.

 

WATU hutegemea mvua ili kufanikisha shughuli mbalimbali, ikiwamo ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi