loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wasanii tungo zenu zilitakiwa kuwa bora zaidi

IJUMAA ya wiki iliyopita ndio yalikuwa maziko ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Magufuli aliyefariki dunia Machi 17, 2012 Dar es Salaam.

Akiwa madarakani, Magufuli alifanya mambo mengi mazuri kwa taasisi na vikundi mbalimbali ambavyo vilionesha kumkubali kutokana na namna alivyo wapigania katika mambo yao.

Moja ya sekta ambazo alizipigania sana Magufuli enzi za uhai wake ni ile ya sanaa. Kwa maana ya muziki na filamu, ambao kiukweli alitumia nguvu zake nyingi kuhakikisha wanapata faida kutokana na kazi wanayoifanya.

Tukiachana na filamu na nyinginezo ebu tuwaangalie hawa wasanii wa muziki wa Bongo Fleva, ambao kwa kiasi kikubwa Magufuli ndio alikuwa akiwapambania ili wanufaike na kazi zao.

Kwa mawazo na mtazamo wangu binafsi, kwa asilimia kubwa wasanii hao wameshindwa kulipa fadhili kwa Rais Magufuli, kutokana na mchango mdogo wa tungo zao wakati wa msiba wake.

Pamoja na wengi kurekodi nyimbo, lakini wachache sana ndio angalau tungo zao zilikuwa na ubora kiasi fulani wakati wengi ni kama walifanya bora liende kwani hazikuwa na ubora.

Wapo wasanii wengi ambao wametunga nyimbo mbalimbali za kumsifu na kumpongeza kutokana na kazi aliyoifanya wakati wa uhai wake, lakini ukweli usiopingika kuwa nyimbo hizo hazikuwa na ubora ule, ambao ulitarajiwa.

Ukimtoa  Peter Msechu ambaye wimbo wake wa ‘Umetuacha Salama’ wengine waliobaki ni kama walifanya ili kuondoa lawama na kujionesha kwamba waliimba nyimbo za kuomboleza.

Wasanii wanatakiwa kuumiza vichwa ili kuibuka na kitu cha maana hasa linapotokea jambo au tukio kubwa kama hilo la kuondokewa na jabari la taifa letu, ambaye pia pamoja na kutetea wanyonge wote, aliwasaidia sana wasanii kupata hai zao.

Magufuli alizinguko katika kampeni zake zote na wasanii wa aina mbalimbali wakati wa kampeni na hakuwaacha nyuma katika shughuli yoyote ya kitaifa inapotokea.

Hivi inamaana wasanii  walizitupa zile kofia ambazo walivalishwa na Magufuli, kipindi cha kampeni na wengine kueleza mbele za umati wa watu kwamba wataziweka kwenye makabati yao ya tuzo kuonesha heshima.

Kitu cha kushangaza zaidi hata ile bendi ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya Tanzania One Theatre au TOT pamoja na kutunga nyimbo mbili, lakini nyimbo hizo hazikuwa na ubora kama ule wa enzi za uhai wa Kapten John Komba.

Hapa nazikumbuka nyimbo zake za maombolezo kwenye msiba wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, ambazo nyimbo zile pamoja na kupita miaka 22, lakini bado nyimbo hizo zinaleta majonzi makubwa pindi zinaposikilizwa.

Pamoja na baadhi ya watu kuwapongezawasanii kwa tungo zao, lakini wazo langu kuwa wangeweza kufanya zaidi kama wangeumiza vichwa vyao na kutoa tungo za uhakika za maombolezo ya Dk Magufuli kwani aliwapigania sana.

Wasanii wanapaswa kubadilika na kuumiza vichwa vyao wakati wakifikiria kurekodi tungo fulani ili kuhakikisha tungo hiyo itakaa vichwani mwa watu kwa miaka mingi, na sio ikipigwa leo kesho imeshasahaulika.

Kwa mawazo yangu binafsi naona wasanii walitakiwa kutunga nyimbo zenye ubora na thamani zaidi kama Magufuli alivyowathamini na kuwajali wakati wa uhai wake.

WATU hutegemea mvua ili kufanikisha shughuli mbalimbali, ikiwamo ...

foto
Mwandishi: Mohamed Akida

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi