loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Kupanda na Kushuka kwa Dk James Mataragio wa TPDC

RAIS Samia Suluhu amemrejesha tena Dk James Mataragio  kuwa Mkurugenzi Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC).

Mataragio ambaye ni mtaalamu wa sekta ya madini, mafuta na gesi asilia amerudishwa leo na kesho ataapishwa Ikulu Dar es Salaam, ikiwa saa chache baada ya Rais Samia kumtangaza Thobias Richard kuwa mkurugenzi mteule wa TPDC.

Mataragio amerejeshwa kwenye nafasi hiyo ambayo ameitumikia kwa miaka saba tangu alipoteuliwa na Rais Mstaafu Jakaya Kikwete Desemba 15, 2014, akiwa ametolewa Houston, Marekani ambako alikuwa akifanya kazi kwenye Kampuni ya Bell Geospace kama ‘Senior Geoscientist’

KUPANDA NA KUSHUKA:

Safari ya Mataragio kwenye utumishi tangu mwaka 2014, imekuwa ya kupanda na kushuka na sasa Rais Samia, ameamua kumteua na kurejea kwenye nafasi hiyo kwa mara nyingine.

Machi 16, 2018- Mataragio na wenzake wanne walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Kisutu na kusomewa shtaka moja la matumizi mabaya ya madaraka.

Ilidaiwa kuwa walibadilisha na kupitisha bajeti na mpango wa ununuzi wa mwaka 2014/2015 na 2015/2016 kwa kuingiza ununuzi wa kifaa cha utafiti cha Airborne Gravity Gradiometer Survey, katika ziwa Tanganyika bila ya kupata kibali cha bodi ya wakurugenzi ya shirika hilo.

Ilidaiwa kwa kufanya hivyo, walikiuka kifungu cha 49(2) cha sheria ya manunuzi ya Umma ya mwaka 2011 huku ikidaiwa kwamba lengo lilikuwa ni kujipatia manufaa yasiyo halali ya Dola 3.2 milioni ambazo ni sawa na Sh7.2 bilioni.

Agosti 24, 2016 Bodi ya Wakurugenzi wa TPDC, ilimsimamisha Mkurugenzi huyo kupisha uchunguzi wa tuhuma zilizokuwa zikimkabili.

JPM AMRUDISHA TENA TPDC

Julai 22, 2019 Hayati Rais John Magufuli aliielekeza wizara ya nishati kumrejesha ofisini katika wadhifa wake aliokuwa nao na kuamuru bodi nzima ya TPDC kuvunjwa.

WASIFU WAKE

Dk Mataragio ana shahada ya uzamili wa maswala ya Maendeleo ya Biashara (MBA) ambayo ameipata Chuo Kuu cha Charlotte, North Caroline, Marekani (2008)

Ana shahada ya Uzamivu- PHD (Geochemistry, Mineralogy, Structural Geology and Petroleum Geology), Chuo Kikuu cha Missouri – Rolla, Missouri, Marekani (2005)

Ana Shahada ya Uzamili Sayansi -MSc (Geochemistry and Petrology), Chuo Kikuu cha Okinawa, Japan (1997)

Ana Shahada ya Sayansi yaani -BSc (Hons) (Geology), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, 1994

UZOEFU WAMBEBA

Mwaka 2004 – hadi sasa, Senior Geoscientist, Bell Geospace Inc, Houston, Texas, USA

2001 – 2004, Mhadhiri Msaidizi, Chuo Kikuu cha Missouri, wakati akisoma Shahada ya Uzamivu

2000 – 2001, Mhadhiri Msaidizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

1999 – 2000, Meneja Mradi, Anglo Gold (Buzwagi)

1994 – 1999, Exploration Geologist, Anglo America Corporation.

Miongoni mwa makampuni makubwa ya kimataifa ya mafuta na gesi aliyofanya nayo kazi kwa niaba ya mwajiri wake Bell Geospace ni pamoja na Petrobras (Brazil); BP; Anadarko; Tullow; Pemex (Mexico); ANP (Brazil), Ecopetrol (Colombia); Petronas, (Malaysia) na Vale Rio Doce.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi