loader
Dstv Habarileo  Mobile
‘Mbali na bandari, tutajenga  karakana ya kukarabatia meli’

‘Mbali na bandari, tutajenga karakana ya kukarabatia meli’

MKUU wa Mkoa wa Tanga, Martine Shigela anaamini kwamba uboreshwaji unaofanywa na serikali katika bandari ya Tanga na zingine Tanzania, utasababisha meli nyingi kubwa kufi ka katika nchi yetu.

Ni kwa msingi, huo, Shigela anaiomba serikali kuona umuhimu wa Tanzania kuwa na karakana maalumu ya kufanyia ukarabati na ujenzi wa meli mpya katika bahari ya Hindi.

Hata hivyo, anapendekeza kwamba ni vyema karakana hiyo ikajengwa Tanga kwa kuwa kuna eneo kubwa la kutosha linaloweza kukidhi haja hiyo. Shigela alitoa rai hiyo wakati Rais Samia Suluhu Hassan (wakati huo akiwa makamu wa Rais) alipotembelea Bandari ya Tanga kukagua ujenzi wa gati na flow meter mwezi uliopita.

“Hakuna sababu ya kuendelea kuwafanyia biashara wenzetu wa nchi jirani wakati tayari eneo la kufanya ukarabati tunalo, hivyo ningeiomba serikali kuona umuhimu wa kulitumia eneo la bandari ya Tanga ili meli zote zinazofika hapa nchini ziweze kuhudumiwa hapa Tanga,” alisema Shigela.

Akijibu hoja hiyo, Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Leonard Chamuriho, alisema Serikali inatarajia kujenga karakana ya kukarabatia meli katika Bandari ya Tanga ili kumaliza changamoto iliyopo nchini ya kufuata huduma hiyo nje ya nchi.

Waziri alisema tayari serikali inaendelea kufanya maboresho makubwa katika bandari zetu nchini kutokana na maelekezo yaliyokwishatolewa ili ziweze kutoa huduma bora ikiwemo kuhudumia shehena kubwa kwa ufanisi.

Alisema Hayati Dk John Magufuli alitoa maelekezo kwa kampuni ya huduma ya meli ije hadi katika mwambao wa ukanda wa Tanga kwa ajili hiyo. “Hivyo tutajenga sehemu ya kuhudumia meli.

Kwa hatua hiyo hakutakiwa na haja ya meli za kwetu kwenda kufanyiwa ukarabati nchi jirani,” alisema Waziri Chamuhilo. Akizungumzia upande wa flow meter aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Bandari Tanzania, Deusdedit Kakoko alisema kuwa wameweza kufunga mfumo wa kuingiza na kutoa mafuta kwenda kwa mteja.

“Tunakamilisha mfumo wa kufunga mafuta ya taa na mafuta ya ndege ili kukamilisha huduma yote kwa urahisi na kuweza kujua mafuta yanayoingia na kutoka,” alisema Kakoko.

Alisema kuwa TPA iko kwenye kutafuta namna ya kumaliza changamoto ya uendeshaji wa mfumo ili ufanywe na serikali mojà kwa moja kwani uliokuwepo ulikuwa unafannywa mwekezaji ambaye ni kampuni ya GBP.

Wakati wa Jukwaa la Biashara mkoani Tanga mwaka 2017, Shigela alisema bandari ya Tanga ilikuwa na shughuli nyingi kulinganisha na kipindi hicho lakini ilivyoanza kulegalega, shehena nyingi ikiwemo ya mikoa ya Kaskazini na Tanga yenyewe ikawa inapitia kwenye bandari jirani ya Mombasa, Kenya.

Hivyo akasema kulikuwa na haja ya kupambana na Bandari ya Mombasa ambayo kwa kipindi hicho ilikuwa inashughulikia mzigo wa tani milioni 28 kwa mwaka wakati Tanzania, tokea Mtwara, Dar es Salaam hadi Tanga ni mzigo wa tani kati ya milioni 16 hadi 17 pekee zilizokuwa zinashughulikiwa.

Tangu maboresho ya bandari zote nchini yafanyike, mzigo unaopitia Tanzania umekuwa ukiongezeka maradufu. Shigela alisema mshindani halisi wa bandari ya Mombasa anapaswa kuwa Bandari ya Tanga na siyo Dar es Salaam na hivyo akasema ili kuongeza ushindani kwa bandari ya Mombasa ni kuboresha bandari ya Tanga.

“Ikumbukwe kwamba bandari ya Mombasa siyo tu kwamba inahudumia mizigo ya nchi ya Kenya bali pia ya Tanzania. Iko mizigo ya Arusha inapitia Mombasa, iko mizigo ya Kilimanjaro, Mnayara na hata ya hapa Tanga,” alisema.

Alisema baadhi ya watu wakati huo walikuwa wakishushia shehena zao Momba na kisha wanapita Horohoro au Horori na kuingiza mizigo yao Tanzania. Alisema sababu kubwa ilikuwa ni meli kubwa kugoma kuja Tanga kutokana kina cha maji kuwa kifupi, tatizo ambalo limekuwa likitatuliwa na tayari meli kubwa zimezanza kufika Tanga bila shida.

Shigela alifafanua kwamba kabla ya upanuzi wa bandari ya Tanga kwa maana ya kuboresha gati na kina, wafanyabiashara wengi wa Tanzania waliokuwa wakishushia mizigo yao Mombasa walihofu mizigo yao kupakuliwa mbali ya gati kwenye tishari, hali inayosababisha gharama mara mbili.

“Kikubwa ninachosema ni kwamba watu wanapenda wakija na meli yao ikikita nanga pale wanashusha mara mioja na kazi inaisha,” alisema Shigela. Mkuu huyo wa mkoa alisema kuna shehena ambayo haiwezi kupitia Dar es Salaam kuja Tanga kama ni mipana sana kutokana na daraja la Wami kuwa finyu na kwamba kabla ya maboresho ya banadti ya Tanga mizigo kama hiyo kama inakuja Tanga ililazimika kupitishiwa Mombasa.

Shigela alisema Tanzania inaweza kunufaika zaidi na Tanga kama itawekeza kwenye bandari hiyo akisema bandari ya Dar es Salaam haina mahala pa kugeuzia meli ndefu sana kama ilivyo kwa Bandari ya Tanga.

“Ukitaka kuipanua bandari ya Dar es Salaam kwa meli ndefu na kubwa kugeuza lazima uiotoe pale ilipo. Lakini hapa Tanga hakuna tatizo kwani kokote ukiingia, kokote unatoka,” alisema.

Alisema kwa kuangalia maneo ya kama ya Tanga, wenzetu wa Kenya wanahangaika kujenga bandari nyingine pale Lamu na lengo lao ni kwenda kwenye kina cha mita 28 baada ya kukamilisha ujenzi wa reli reli ya viwango vya kisasa (standard gauge).

“Wanalenga kukamata mizigo, siyo ya Uganda pekee bali pia ya Kongo, Rwanda na Burundi. Na kwa kweli hapa Tanga tukifanikiwa mambo matatu tutaipaisha nchi yetu na tutakuwa washindani halisi wa bandari ya Mombasa.

Mambo hayo ni kupanua bandari, reli na barabara ya kutoka Handeni, Kilindi, Kibirashi kwenda Singida. Ukiwa na barabara hiyo unapunguza zaidi ya kilometa 150 kwenda Dar es Salaam kutokea Singida kuja Tanga.” alisema.

Akaongeza: “Ukifungua njia ya reli Tanga, utakuta kwamba hakuna malori yanayobeba mizigo kwenda Dar es Salaam na kusababisha msonagamano wa magari usio wa lazima.

Lakini utakuwa tayari umejenga mazingira ambayo watu hawatakuwa na sababu ya kwenda Mombasa kwani mizigo mingi itakuja anga,” alisema.

https://www.apps.tsn.go.tz/public/uploads/d591f9e6c37dadf5d077ba646b0300ed.jpg

WAFUGAJI wa ng'ombe wa maziwa nchini wamekuwa wakikabiliwa na changamoto ...

foto
Mwandishi: Amina Omari

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi