loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Joshua ajipanga kumvaa Fury

MRATIBU wa pambano la bondia, Antony Joshua, Eddie Hearn amethibitisha kuwa bondia huyo ameanza kujiandaa kwa pambano dhidi ya Tyson Fury, ambalo tarehe na sehemu litakapofanyika itatangazwa wiki ijayo.

Amesema mabondia Fury na Joshua wamesaini mkataba wa kupigana mapambano mawili wenye thamani ya pauni milioni 200 ambazo ni zaidi ya Sh bilion 643.

Hearn alisema Joshua amejipanga kwenda kuweka kambi ya mazoezi kwenye chuo cha michezo mjini Sheffield na mkufunzi wake, Rob McCracken.

Mratibu huyo alisema mpaka wiki ijayo mipango yote ya pambano hilo litafanyika wapi na lini itakuwa imekamilika.

Mabondia hao wawili wanashikilia mikanda yote ya uzito wa juu, Antony Joshua anashikilia mikanda minne ya uzito wa juu ambayo ni WBA, IBF, WBO na IBO, wakati Tyson Fury anashikilia mkanda wa WBC.

Kwa kigezo cha mabondia kutoka Uingereza kushikilia mikanda yote ya uzito wa juu, pambano hilo linatajwa kuwa kubwa kwenye historia ya mchezo wa masumbwi nchini humo.

KLABU ya soka ya Simba imeingia mkataba ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi