loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Corona yaahirisha French Open

MASHINDANO maarufu ya tenisi ya French Open yameahirishwa kutokana na kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya corona nchini Ufaransa.

Waziri wa michezo wa nchi hiyo, Roxana Maracineanu amesema serikali iliweka kizuizi cha tatu Jumamosi iliyopita, ambapo Rais Emmanuel Macron alisema kitamalizika katikati ya Mei wakati mashindano hayo yanapaswa kufanyika Roland Garros kuanzia Mei 23 hadi Juni 6.

 

Mashindano hayo yalikuwa awali yafanyike mwaka jana, lakini yaliahirishwa hadi majira ya joto kwa sababu ya janga la corona.

"Tunazungumza na Shirikisho la Tenisi la Ufaransa kuona ikiwa tunapaswa kubadilisha tarehe na uwezekano wa kuanza tena kwa michezo yote," Maracineanu aliambia redio ya nchi hiyo.

"Leo ingawa mchezo wa kiwango cha juu umehifadhiwa, tunajaribu kupunguza hatari za kueneza virusi ndani ya michezo kwa wachezaji."

Ufaransa ina wagonjwa 5,000 wa corona katika vitengo vya wagonjwa mahututi.

Ijumaa iliyopita nchi hiyo  ilirekodi wagonjwa wapya 46,677 na vifo 304.

KLABU ya soka ya Simba imeingia mkataba ...

foto
Mwandishi: PARIS, Ufaransa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi