loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

De Ligt ajuta Juventus

BEKI wa kati wa Juventus, Matthijs De Ligt amesema anajuta kusaini Juventus na kuacha timu nyingine kubwa zilizomuhitaji kama Manchester United na Barcelona.

De ligt alikuwa kwenye kiwango cha juu katika msimu wa mwaka 2018/2019 akiwa na Ajax Amsterdam ambapo walifanikiwa kucheza nusu fainali ya klabu bingwa Ulaya wakatolewa na Tottenham kwa mabao 3-2.

Ajax ilikuwa na wachezaji vijana wazawa wa Uholanzi waliokuwa katika kiwango bora akiwemo Frankie de Jong aliyejiunga na Barcelona, Dony van de Beek ambaye baadaye alitimkia Manchester United.

Kizazi chao kimetawanyika katika ligi tatu tofauti barani Ulaya ambazo ni EPL, La Liga na Serie A ambako hakijapata mafanikio makubwa kama watu walivyotarajia, hali inayomfanya ajute uwepo wake Juventus.

De Ligt amefanikiwa kuchukua ubingwa wa Serie A akiwa na Juventus katika msimu wa 2019/2020, lakini kwa sasa hana furaha na maisha ya Turin, huku hamu ya kujiunga na Barcelona ikiwa kubwa kwa sababu ya uwepo wa kocha Ronald Koeman.

Mwenendo wa Juventus kwa sasa si mzuri kwani wapo katika nafasi ya nne wakiwa na pointi 56 katika michezo 28 waliocheza, huku Inter Milan wakiongoza ligi wakiwa na pointi 68 ikiwa nyuma na imebaki michezo 10 tu.

KLABU ya soka ya Simba imeingia mkataba ...

foto
Mwandishi: TURIN, Italia

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi