loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Martial nje akiuguza goti

MSHAMBULIAJI wa Manchester United na timu ya taifa ya Ufaransa, Anthony Martial huenda akakosa michezo yote ya msimu huu baada ya vipimo kuonesha ameumia sana kwenye goti na atakuwa nje kwa kipindi kirefu.

Martial alipata majeraha hayo akiwa na timu yake ya taifa ya Ufaransa kwenye mchezo dhidi ya Kazhakstan ambapo alitengeneza bao la kwanza kabla ya kufanyiwa mabadiliko kutokana na maumivu hayo.

Kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjear alisema wanahitaji kufanya kazi ya ziada kuziba pengo la mchezaji huyo ambaye pia atashindwa kushiriki michuano ya Mataifa ya Ulaya ya mwaka 2020 kama bado atakuwa hajapata nafuu hadi mwishoni mwa Mei.

Martial ameifungia klabu yake mabao saba na kutengeneza mengine nane kwenye michezo 36 aliyoicheza toka kuanza kwa msimu huu.

TIMU ya Mbeya City imetumia vema ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi