loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Rais Samia awapa shavu wasanii, wanamichezo

RAIS Samia Suluhu Hassan ameitaka Wizara ya Habari,  Utamaduni, Sanaa na Michezo kutatua changamoto za wasanii na wanamichezo ili wajiajiri.

Rais Samia aliyasema hayo jana Ikulu, Dar es Salaam alipokuwa akiwaapisha makatibu wakuu wa wizara na viongozi mbalimbali wa serikali aliowateua hivi karibuni.

"Wasanii na wanamichezo ni ajira, hivyo tukiwapa nguvu na kutatua changamoto zao, vijana wengi wataweza kujiaajiri . Hivyo naomba mkaliangalie hilo kwa mapana, " alisema. 

Rais Samia ni miongoni mwa viongozi aliyekuwa karibu kufuatilia maslahi ya wasanii na wanamichezo tangu akiwa Makamu wa Rais chini ya uongozi wa Rais John Magufuli aliyefariki Machi 17 na kuzikwa kijijini kwake, Chato Machi 26 mwaka huu.

Aidha, akiwa Makamu wa Rais, alikuwa mlezi wa timu ya soka ya taifa ya wanawake.

Akizungumza sababu za kumteua Naibu Waziri wa michezo mwanamke, Pauline Gekul wiki iliyopita, Rais Samia alisema amefanya hivyo kwasababu wanawake wanafanya kazi kubwa kwenye michezo lakini hawatambuliwi kama ilivyo kwa wanaume.

Pauline anachukua nafasi ya Abdallah Ulega aliyehamishiwa Wizara ya Mifugo.  Mwanamama huyo sasa atafanya kazi na Waziri, Innocent Bashungwa kwenye wizara hiyo.

KOCHA wa Simba, Didier Gomes na wa Yanga, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi