loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Tanzanite bado inatoroshwa, Samia azuia Kitalu C

PAMOJA na kujenga ukuta wenye urefu wa kilometa 24.5 katika eneo la machimbo ya madini ya tanzanite, Mirerani wilayani Simanjiro mkoani Manyara ili kudhibiti utoroshwaji wake, bado kuna utoroshaji wa madini hayo.

Kutokana na hali hiyo, Rais Samia Suluhu Hassan, ameagiza Wizara ya Madini kuimarisha ulinzi zaidi ili kuzuia kabisa utoroshaji huo wa madini ya tanzanite ambayo kwa duniani nzima yanayopatikana nchini Tanzania peke yake.

Sambamba na hilo, Rais amepiga marufuku walioanza kugawa vitalu katika eneo la Kitalu C waache mara moja kwa kuwa eneo hilo ni la akiba, lisiguswe kwa sasa.

Alitoa agizo hilo jana Ikulu, Dar es Salaam, katika hafla ya kuwaapisha makatibu wakuu, naibu makatibu wakuu na wakuu wa taasisi za serikali aliyowateua Aprili 4, mwaka huu.

“Tumejenga ukuta kama kilometa zaidi ya 24 tukaweka na majeshi, CDF (Mkuu wa Majenzi ya Ulinzi na Usalama) yuko pale, lakini ndugu zangu madini yanatoroshwa kama mwanzo,” alisema Rais Samia.

Aliongeza, “Tukibahatika kuliona tunapiga picha na Rais, hili hapa bonge la tanzanite lakini hatujui ni mangapi yamepitishwa chini kwa chini.”

Aliagiza ulinzi zaidi uongezwe Mirerani, ‘si wa bunduki za CDF’ bali aliwataka watumie ujuzi wanaoujua kulinda wachimbaji wasitoroshe madini hayo kwani CDF kupitia Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) analinda juu na wao walinde na kuwadhibiti wanaopita chini kwa chini na kutorosha madini hayo.

“Naomba sana Mererani mkapasimamie vizuri, madini yetu haya ndio tegemeo letu kwenye nchi, tusipoyasimamia vizuri tunaangusha wenyewe uchumi wetu.

“Madini mnafanya vizuri lakini je mmeongeza usimamizi vizuri? Mngeweza kuwa wa kwanza katika kuchangia Pato la Taifa, lakini sasa sijui ni wa pili au watatu hivi. Ongezeni usimamizi eneo hilo,” alisisitiza.

Kuhusu Kitalu C, alisema kuna watu wameanza kuvamia na kugawana vitalu hapo. Aliwaagiza waache mara moja kwa kuwa kitalu hicho ni akiba.

Ukuta wa Mererani ulianza kujengwa mwaka 2017 na kuzinduliwa na aliyekuwa Rais, Dk John Magufuli Aprili mwaka 2018. Ulitumia gharama za Sh bilioni sita na una kamera za ulinzi zipatazo 306.

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, ...

foto
Mwandishi: Gloria Tesha

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi