MADEREVA wa magari na waendesha bodaboda mjini Tanga na baadhi ya vijiji wamelazimika kununua mafuta ya petroli kwa kati ya Sh 2,400 na Sh 2,500 kwa lita moja kutoka kwa wauzaji wa mitaani baada ya nishati hiyo kuadimika kwa siku mbili kwenye vituo vya mafuta.
Bei halisi ya petroli katika vituo vya mafuta ni Sh 2,087 kwa lita moja.
Mwandishi wa habari hii juzi alishuhudia misururu ya waendesha bodaboda wakihangaika kupanga foleni kutafuta mafuta kwenye kituo kimoja cha mafuta na wengine wakihangaika kutafuta kwa wauzaji wa mitaani.