loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Watu 14 wafa ajalini Kenya

WATU 14 wamekufa katika ajali ya barabarani iliyohusisha magari mawili ya abiria yaliyogongana uso kwa uso katika eneo la Kwa Shume karibu na mji wa Kizingo katika barabara kuu ya Malindi – Mombasa.

Kwa mujibu wa mamlaka nchini Kenya, ajali hiyo iliyotokea jana ilihusisha basi la  Muhsin na jingine la Sabaki ambayo yanafanya safari zake katika kaunti ya Kilifi.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Kaunti ya Malindi, Joab Gayo amethibitisha kupokea miili ya watu 14 na kupelekwa moja kwa moja katika chumba cha kuhifadhia maiti ili kuihifadhiwa.

Baada ya taarifa za ajali hiyo kuenea, wananchi walijitokeza katika hospitali hiyo katika eneo la kuhifadhi maiti ili kutambua miili ya ndugu zao kwa ajili ya kuichukua kwa maziko.

Dk Gayo aliwaambia waandishi wa habari kuwa, majeruhi waliofikishwa katika hospitali hiyo ni 18, huku 14 wakiwa wanaume na wanne wanawake. Alisema kati ya majeruhi wote, sita kati yao hali zao zilikuwa mbaya.

Kamishna wa Kaunti ya Kilifi, Kutwa Olaka alisema basi la Muhsin lilikuwa likitokea Mombasa kwenda Garsen, wakati basi la Sabaki lilikuwa likitoka Malindi kwenda Mombasa.

 

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: MOMBASA, Kenya

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi