loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Simba wapania ushindi Misri

 

MLINZI kisiki wa kimataifa wa Kenya na  klabu ya Simba, Joash Onyango amesema malengo yao msimu huu ni kushinda michezo yote ya hatua ya makundi na kuingia  robo fainali wakiwa vinara wa Kundi A, hivyo Al Ahly wasitarajie mteremko.

Simba itashuka uwanjani kesho nchini Misri kuwakabili Al Ahly ambao wanashika nafasi ya pili katika msimamo wa Kundi A wakiwa na pointi nane.

Akizungumza jana, Onyango nyota wa zamani wa Gor Mahia, alisema licha ya kuwa wamefuzu hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika,  hawatakubali kupoteza mchezo wao wa mwisho wa kumaliza hatua ya makundi na kuchafua rekodi yao.

Alisema ubora wa kikosi chao unatokana na malengo waliyojiwekea pamoja na umoja uliopo katika kikosi hicho ambacho kinashika nafasi ya pili katika orodha ya timu 16 bora za Ligi ya Mabingwa msimu huu.

“Tumefuzu hatua ya makundi lakini hii haitufanyi tuingie katika mchezo huu tukiwa tumeridhika tunaenda kupambana ili kutimiza malengo yetu ya msimu huu,” alisema Onyango.

Simba wanaingia katika mchezo ujao wakiwa na kumbukumbu nzuri dhidi ya Al Ahly, baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa awali uliofanyika katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kwa bao lililofungwa na kiungo mshambuliaji Luis Miquissone.

Wakati huohuo, kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba raia wa Zambia, Clatous Chota Chama ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa wiki na kuwabwaga, Amir Sayoud wa CR Belouizdad ya Algeria, Ricardo Goss wa Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini na Ferjani Sassi Zamalek FC ya Misri.

Chama anakuwa mchezaji wa pili kutoka Simba SC kutwaa tuzo hiyo baada ya Luis Miquissone kufanya hivyo baada ya mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara kuwafunga Al Ahly.

Wakati huohuo, Simba imetua salama jijini Cairo, Misri tayari kwa mchezo huo wa mwisho wa hatua ya makundi.

KOCHA wa Simba, Didier Gomes na wa Yanga, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi