loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Mwambusi  aridhika na kikosi chake

BAADA ya klabu ya Yanga SC kuibuka na ushindi wa  mabao 3-0 dhidi ya African Lyon, Kocha Mkuu wa timu hiyo, Juma Mwambusi amesema ameridhishwa na kiwango kilichooneshwa na kikosi chake.

Mwambusi alisema ushindi huo wa mabao 3-0 umerudisha morali katika kikosi chake ambacho kinasaka taji la Ligi Kuu Tanzania Bara ambalo hawajalitwaa kwa misimu mitatu mfululizo.

Mara ya mwisho Yanga kushuka uwanjani ilikuwa Machi 7  katika Uwanja wa Ushirika Moshi na kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Polisi Tanzania.  

Yanga itaingia katika mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara ikiwa kileleni mwa msimamo ikiwa na pointi 50 na imeshuka uwanjani mara 23.

Akizungumza na HabariLEO jana, Mwambusi alisema amefurahishwa na kiwango kilichooneshwa na vijana wake katika mchezo huo wa kirafiki ambao ulikuwa wa kuangalia wapi kuna mapungufu ayafanyie kazi kabla ya kuwakaribisha KMC katika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jumapili hii.

“Nilikuwa nahitaji mchezo wa kirafiki ili kuangalia ubora wa wachezaji wangu ambao kwa muda mrefu hawakupata mchezo wa kujipima nguvu, licha ya ushindi nimeyaona baadhi ya mapungufu ambayo nitayafanyia kazi kabla ya mchezo ujao,” alisema.

Kocha huyo alisema huu ni wakati muhimu zaidi kwao katika kulisaka taji hivyo wanahitaji umakini mkubwa ili kuhakikisha wanachukua pointi tatu katika kila mchezo ili kuongeza wigo wa pointi kileleni na kutwaa ubingwa.

KOCHA wa Simba, Didier Gomes na wa Yanga, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi