loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

CAG: Milioni 172 zilienda Kigwangalla 'Kill Challenge'

Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali imeonyesha kuwa, Waziri wa Maliasili na Utalii alizielekezea Hifadhi za Taifa za Ngorongoro na Tanapa kulipa shilingi milioni 172 kwa ajili ya kugharamia shindano la Kigwangala Kill Challenge kuhamasisha wasanii kupanda mlima Kilimanjaro.

Akitoa ripoti hiyo CAG, Charles Kichere amesema kuwa utaratibu huo ulikuwa nje ya bajeti ya taasisi hizo na hakukuwa na risiti za Malipo na hivyo kusababisha hasara kwa Serikali.

Taarifa ya CAG inaeleza kuwa kulikuwa na maagizo na maagizo ya Waziri wa Maliasili na Utalii kuelekeza malipo kwa Kampuni ya Wasafi, baada ya mahojiano Waziri alisema, kampuni ya Wasafi iliomba zabuni.

Amefafanua kuwa shilingi milioni 140 zilizolipwa hazikuendana na sheria za matumizi ya fedha za umma.

“Wizara ililipa milioni 140 kwa kampuni ya Wasafi kwaajili ya wasanii ambao wangetangaza utalii wa ndani katika mikoa sita, hata hivyo hakukuwa na mkataba wowote uliosainiwa baina ya wizara na kampuni ya Wasafi na kushindwa kuhakiki wigo na huduma iliyotolewa na kampuni ya Wasafi.” Amesema Kichere

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: Rahimu Fadhili

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi