loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Wafanyakazi zaidi ya 1500 SGR hawana vibali

Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) ya miradi ya maendeleo imeonyesha kuwa wafanyakazi 1,538 kati ya 2,408 wa raia wa kigeni wanaojenga reli ya kisasa kipande cha kwanza na pili kutoka Dar es Salaam hawakuwa na vibali vya kazi.
Ripoti hiyo ya mwaka wa fedha unaoishia Juni 20, 2020 iliyotolewa leo inaeleza kuwa hali hiyo ni kinyume na Kifungu cha 9 (2) (a) cha Sheria za Ajira za Raia wa Kigeni ya mwaka 2015.

“Mapitio ya ripoti ya maendeleo ya kazi ya mwezi wa Novemba 2020 yalibaini kuwa jumla ya raia wa kigeni 586 kati ya 924 walioajiriwa kwenye kipande cha kwanza cha ujenzi wa reli ya kisasa hawakuwa na vibali vya kufanya kazi.”

“Hali hii pia ilibainika kwenye kipande cha ujenzi cha pili ambapo ilibainika kuwa jumla ya raia wa kigeni 952 kati ya 1,484 hawakuwa na vibali vya kufanya kazi,” inaeleza ripoti hiyo ya miradi ya maendeleo.

Ripoti inabainisha kuwa kutozingatiwa kupata vibali vya kazi kulisababisha kutolipwa kwa ada ya vibali vya kazi inayofikia Dola za Marekani 1,538,000 ambazo ni sawa na Sh3,537,400,000 (kiwango cha ubadilishaji kilichotumika ni 2,300).

“Mahojiano zaidi na maafisa wa TRC (Shirika la Reli Tanzania) yalionesha kuwa idara ya uhamiaji ilitoa idhini ya raia hao wa kigeni kutumia visa ya biashara kuendelea kufanya kazi wakati maombi yao ya vibali vya kazi yakishughulikiwa.”

“Hata hivyo, ilielezwa wazi katika barua hiyo kwamba kutolewa kwa viza ya biashara hakikuwa kisingizio cha kutokuwa na vibali vya kufanya kazi kwa raia hao wa kigeni walioajiriwa katika mradi wa SGR,” imesema ripoti hiyo.

CAG pia amebainisha kuwepo kwa raia wa kigeni 1,026 wanaofanya kazi katika mradi wa SGR (kwa vipande vyote viwili) wasio na vyeti vya sifa zao za masomo.

“Ripoti ya Maendeleo ya kazi ya mwezi wa Novemba 2020 ilionesha kuwa, vyeti vyao vilikuwa vikiendelea na michakato anuwai ya uthibitishaji. Hata hivyo, asilimia 83 kati yao walikuwa wakisubiri kwa sababu ilibainika waombaji hawakuwa na vyeti halisi vya masomo na walikuwa wakingojea kuvipokea kutoka Uturuki,” ameeleza.

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: Rahimu Fadhili

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi