loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

CAG: Kampuni ya Wasafi ililipwa kinyume na sheria

Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) imebaini ubadhilifu wa fedha katika Wizara ya Maliasili na Utalii ambapo ripoti inaeleza kuwa shilingi milioni 140 zililipwa kwa Kampuni ya Wasafi kinyume na Sheria ya Matumizi ya Umma.

Kupitia ripoti hiyo imefahamika kuwa fedha hizo zililipwa kwa ajili ya wasanii wa kampuni hiyo kutangaza utalii wa ndani katika mikoa sita ya Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Dodoma, Moshi-Kilimanjaro na Iringa.

“Nilibaini wizara ililipa shilingi milioni 140  Kampuni ya Wasafi kwa ajili ya wasanii ambao wangetangaza utalii wa ndani, hakukuwa na mkataba wowote uliosainiwa kati ya kampuni hiyo na wizara, hivyo sikuweza kuhakiki wigo wa kazi pamoja na huduma zilizotolewa na Kampuni ya Wasafi,”ilieleza ripoti hiyo.

“Kulikuwa na maagizo ya waziri (Dk Hamis Kigwangala) yakielekeza malipo kwa Kampuni ya Wasafi, katika mahojiano waziri alikiri kuwa, kampuni hiyo iliomba zabuni ya kutangaza tamasha hilo katika mikoa iliyotajwa na kutoa maagizo ya kutolewa malipo hayo.”

Amesema kwa maoni yake kiasi cha shilingi milioni 140  walicholipwa Wasafi kufuatia malekezo hayo, hakiendani na sheria ya matumizi ya umma.

JOPO la Majaji 12 nchini Marekani limemtia hatiani ...

foto
Mwandishi: Vicky Kimaro

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi