loader
Simba, Al Ahly kulinda heshima

Simba, Al Ahly kulinda heshima

WAWAKILISHI wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba leo  itawakabili Al Ahly katika Uwanja wa AL-Salam Misri, mchezo wa kukamilisha ratiba hatua ya makundi .

Simba vinara wa Kundi A wakiwa na pointi 13 inakwenda katika mchezo huo ikiwa haina cha kupoteza baada ya kuingia hatua ya robo fainali ikiwa kileleni mwa msimamo.

Wekundu wa Msimbazi wanakutana na Al Ahly, wakiwa na kumbukumbu nzuri ambapo walichukua pointi tatu mbele ya mabingwa hao watetezi wa taji hilo baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Akizungumza jana kocha mkuu wa Simba, Didier Gomes, alisema anawaheshimu Al Ahly kwani ni timu kubwa na imekuwa ikifanya vizuri inapokuwa nyumbani  lakini malengo yao ni kumaliza vizuri hatua ya makundi  jambo linaloongeza ugumu wa mchezo huo licha ya timu zote kuingia hatua ya robo fainali.

“Najua Al Ahly  hawatakubali kupoteza mara mbili dhidi yetu watataka kuonesha ubora wao tuko tayari kwa mapambano,  kikosi changu kiko kamili wachezaji wote wako vizuri,” alisema Gomes.

Naye nahodha wa Simba, John Bocco, alisema kuwa wameenda Misri  kupambana na kurudi na ushindi hivyo Al Ahly wanajua haitakuwa mechi rahisi kwao utakuwa mchezo mgumu lakini wamejipanga kuhakikisha wanashinda ili kuongeza hali ya kujiamini.

“Tumefanya maandalizi ya kutosha naamini tutakwenda kupata matokeo mazuri kutokana na morali iliyopo kikosini na tumejipanga kuhakikisha tunaondoka na pointi tatu, tulipata matokeo katika mchezo wa mwisho naamini tutaendeleza tulipoishia,” alisema Bocco.

Simba na Al Ahly zimefuzu hatua ya robo fainali kwa tofauti ya pointi tano hivyo endapo Al Ahly itashinda bado haitaishusha Simba kileleni.

Timu hizo katika michezo mitano ya mwisho kukutana, Simba imeshinda mara mbili na imefungwa mchezo mmoja, lakini michezo yote imeshinda nyumbani na mchezo wa mwisho waliocheza Misri, wenyeji Al Ahly waliifunga mabao 5-0 mwaka 2019 ndio maana Simba wanasema wanakwenda kulipa kisasi.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/d5a04319e7635bfcf8d7056fc0011819.jpeg

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu ...

foto
Mwandishi: Martin Mazugwa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi