loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Ligi yarejea kwa sare

LIGI Kuu Tanzania Bara inaonekana kuwa ngumu baada ya timu zote kugawana pointi katika michezo iliyochezwa jana.

Ligi ilikuwa imesimama kwa takribani wiki tatu kwa ajili ya maombolezo ya kifo cha Rais John Magufuli kilichotokea Machi 17 na kupisha mechi za kimataifa za kufuzu Afcon. 

Katika mchezo uliochezwa mapema saa 8:00 Mbeya City na Kagera Sugar zimeshindwa kutambiana baada ya kutoka suluhu kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Sokoine Mbeya.

Kwa matokeo hayo Kagera Sugar inashika nafasi ya 13 ikiwa na pointi 26 baada ya kucheza michezo 25 na Mbeya City inashika nafasi ya 16 ikiwa na pointi 21 baada ya kucheza michezo 24.

Namungo ikiwa nyumbani ililazimisha sare na Ihefu katika Uwanja wa Kassim Majaliwa, Ruangwa, Lindi.

Ihefu walikuwa wa kwanza kupata bao dakika ya 22 likifungwa na Raphael Loth akimalizia kona iliyopigwa na Omar Mkono na dakika ya 60 Ibrahim Ali aliisawazishia Namungo akiunganisha krosi ya Stephen Sey.

Kwa matokeo hayo Ihefu imebaki katika nafasi yake ya 17 ikiwa na pointi 21 baada ya kucheza michezo 25 na Namungo ikiwa katika nafasi ya 10 ikiwa na pointi 28 baada ya kucheza michezo 19.

KOCHA wa Simba, Didier Gomes na wa Yanga, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi