loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Waziri Ardhi: Tunapokea maoni, ushauri tozo uhamisho ardhi

SERIKALI imesema kuwa iko tayari kupokea maoni na ushauri ywa wadau kuhusu viwango vya tozo zinazohusu uhamisho wa miliki za ardhi na tozo nyingine zinazohusu sekta ya ardhi kwa ujumla ili kuboresha huduma kwa Wananchi.

Hayo yamesema  na Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi, Dk Angelina Mabula alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Nyasa, Stella Manyanya kwa niaba ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi aliyetaka kujua mpango wa serikali katika kuboresha gharama za kuhamisha umiliki wa ardhi.

Dk Mabula alisema uhamishaji wa milki za ardhi huzingatia Sheria ya Ardhi (Sura 113), Sheria ya Usajili wa Ardhi (Sura 334), Sheria ya Ushuru wa Stempu (Sura 189) na Sheria ya Kodi ya Mapato (Sura 332) ambayo inahusika na Kodi ya Ongezeko la Mtaji. 

“Kwa mantiki hiyo, Wizara yangu inasimamia gharama za Ada ya Uthamini, Ada ya Upekuzi katika Daftari la Msajili, Ada ya Maombi ya Uhamisho wa Milki na Ada ya Usajili ambazo ni gharama nafuu na wananchi wa kawaida wanaweza kuzimudu.

“Wizara yangu katika nyakati tofauti imekuwa ikiboresha gharama za uhamishaji na umilikishaji ardhi nchini. Kwa mfano, katika mwaka wa fedha 2018/19 gharama ya tozo ya mbele (premium) ilipunguzwa kutoka asilimia 7.5 hadi asilimia 1 ya thamani ya ardhi ambayo hutozwa mara moja tu wakati wa umilikishaji ardhi kwa maeneo ya urasimishaji mijini na hadi asilimia 2.5 kwa maeneo mengine,” alisema 

 Aidha, alisema kuwa Wizara imeboresha gharama za Urasimishaji kwa kupunguza kutoka Sh 250,000 hadi Sh 150,000 na Halmashauri zingine zinatoza hadi Sh 50,000.

SERIKALI imezuia ndege zote zinazofanya safari za kwenda ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu, Dodoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi