loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Waua, wakata kichwa na kukimbia nacho

MTU mmoja aliyefahamika kwa jina la Shinze Mugalama (50) ameuawa na watu wasiojulikana kwa kukatwa shingo na kitu chenye ncha kali kisha wauaji kukimbia na kichwa cha mtu huyo.

Tukio hilo limetokea katika Tarafa ya Manyovu wilayani Buhigwe mkoani Kigoma.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma, James Manyama alisema tukio hilo limetokea juzi katika Kijiji cha Kanda, wilaya ya Buhigwe, mkoa Kigoma Nyumbani kwa Pausta Mugalama eneo alipokuwa amelala marehemu. Pausta ni dada wa Shinze (marehemu).

Alisema kuwa kutokana na tukio hilo watu wawili wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano na majina yao yamehifadhiwa kwa ajili ya uchunguzi wa zaida ili kutambua wahusika wote wa tukio hilo.

Baadhi ya wananchi wamelaani kitendo hicho na kuliomba jeshi la polisi kuongeza jitihada za kupambana na uhalifu hasa kwa kushirikisha wananchi kutoka maeneo husika.

Mkurugenzi wa asasi isiyo ya kiserikali ya maendeleo ya wanawake Kigoma (KIWODE), Sophia Nassibu aliiomba mamlaka husika zichukuwe sheria kwa wahusika wa vitendo hivyo vya ukatili.

Ofisa Ustawi wa jamii, Manispaa ya Kigoma Ujiji, Agness Punjila alisema mauaji hayo ni matokeo ya kuongezeka kwa vitendo vya ukatili kwa jamii

“MTU niliyefanya naye mahojiano alikuwa anafanya kazi kwenye ...

foto
Mwandishi: Fadhili Abdallah, Kigoma

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi