loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Dodoma, Gwambina kicheko

TIMU ya Dodoma Jiji imeondoka na pointi tatu katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Tanzania Prisons uliochezwa Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga.

Katika mchezo huo timu zote zilimaliza kipindi cha kwanza bila kufunga lakini kipindi cha pili Dodoma jiji walikuja na kasi na kupata bao dakika ya 54 likifungwa na Dickson Ambundo.

Kwa matokeo hayo Dodoma Jiji imefikisha pointi 37 baada ya kucheza michezo 25 na Prisons inabaki na pointi 31 katika nafasi ya tisa baada ya michezo 24.

Katika mchezo wa pili uliochezwa Uwanja wa Gwambina Complex wenyeji Gwambina waliifunga Coastal Union kwa mabao 4-0.

Mabao ya Gwambina yalifungwa na Meshack Abraham dakika ya tisa, Paul Nonga dakika ya 31, Rajab Athuman dakika ya 37 na Jimson Mwanuke dakika ya 75.

Kwa matokeo hayo Gwambina imefikisha pointi 30 baada ya kucheza michezo 23 na Coastal Union inabaki na pointi zake 27 baada ya kucheza michezo 24.

KOCHA wa Simba, Didier Gomes na wa Yanga, ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi