loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

City yavutwa shati

BAO la ushindi la Leeds lilifungwa na Dallas Stuart dakika za majeruhi na limepunguza kasi ya Manchester City kuwania ubingwa wa Ligi Kuu England baada ya kukubali kichapo cha 2-1 kwenye Uwanja wa Etihad.

Huo ni ushindi bora wa Leeds tangu waliporejea tena Ligi Kuu na tafsiri yake sasa kama Manchester United itashinda mechi zake mbili zinazofuata dhidi ya Tottenham na Burnley watapunguza tofauti ya pointi dhidi ya Man City kuwa nane.

Kama itakuwa hivyo City watalazimika kupata pointi 11 katika mechi zao sita zilizosalia kushinda taji lao la tatu katika misimu minne.

Haikuwa rahisi kwa Leeds inayonolewa na Marcelo Bielsa kuibuka na ushindi huo kutokana na kucheza pungufu kwa muda mrefu baada ya nahodha wake Liam Cooper kuoneshwa kadi nyekundu kwa kumchezea rafu Gabriel Jesus.

Dallas aliitanguliza Leeds kwa kufunga bao dakika tatu kabla ya mapumziko kwa shuti hafifu lililojaa wavuni hata hivyo City walioutawala mchezo kwa muda mrefu walilazimika kusubiri mpaka dakika ya 76 kusawazisha bao likifungwa na Ferari Torres.

Dallas aliifungia tena Leeds bao la ushindi dakika za majeruhi akitumia vyema pasi ya Ezgjan Alioski na kupiga mpira uliompita kipa Ederson wa City.

KOCHA wa Simba, Didier Gomes na wa Yanga, ...

foto
Mwandishi: LONDON, England

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi