loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

TSC: Walimu mkionewa msikae kimya

TUME ya Utumishiwa Walimu (TSC) imeshauri walimu wazitumie ofi si za tume hiyo kuwasilisha kero na changamoto za kiutumishi katika maeneo ya kazi ili zipatiwe ufumbuzi kwa wakati. Mkurugenzi wa Ajira, Maadili na Maendeleo ya Walimu TSC, Christina Hape, alitoa ushauri huo katika kikao kazi cha walimu wa shule za msingi na sekondari wa Wilaya ya Same.

Alisema serikali ilianzisha TSC ili kusaidia walimu kutatua kero zao na kuwawezesha kutekeleze majukumu ya kufundisha wanafunzi katika mazingira ya amani na utulivu.

“TSC ipo kwa sababu walimu mpo, tunafanya kazi kwa kuwa ninyi mpo, sisi ni watumishi wenu na tuna wajibu wa kuhakikisha uwepo wetu unawasaidia ninyi kufanya kazi zenu kwa ufanisi. Tupo kwa ajili ya kufanya walimu wafanye kazi kwa furaha na amani,” alisema.

Alisema baadhi ya viongozi wamegeuka kuwa miungu watu kwa kuwa wamekuwa wakiwanyanyasa walimu wanapofika kwenye ofisi zao kupata huduma zilizowekwa kwa mujibu wa sheria.

“Kuna baadhi ya viongozi wakimuona tu mwalimu ameingia ofisini kwake hata kabla ya kumsikiliza, anaaza kumfokea na kumkaripia mpaka mwalimu anapoteza ujasiri wa kujieleza.

Mwingine anagoma kupitisha barua ya mwalimu kwa makusudi tu ili amkomoe mwalimu, bila kuelewa kuwa kufanya hivyo ni kuvunja sheria,” alisema Hape.

Alisema mwalimu ni mtumishi wa umma kama walivyo watumishi wa kada nyingine, hivyo anastahili kuheshimiwa na kuhudumiwa vizuri sehemu yoyote anapoingia ilimradi hajavunja sheria na taratibu za utumishi.

Hape alisema, mwalimu anapokwenda katika ofisi ya umma kwa masuala ya kiutumishi na akaona ametendewa kinyume na utaratibu, asikae kimya, bali awasilishe malalamiko katika ofisi za TSC ili hatua zichukuliwe haraka na haki yake ipatikane haraka.

“Mwalimu unapaswa kumheshimu kiongozi wako, lakini si kumwogopa. Miongoni mwa majukumu ya TSC kwa mujibu wa sheria, ni kushughulikia malalamiko ya walimu.

Hivyo, pale unapotendewa ndivyo sivyo usikae kinyonge, leta malalamiko yako sisi tutawasiliana na mamlaka inayohusika na utapata haki yako,” alisema. Aliwataka walimu wilayani humo kuzingatie nguzo za maadili ya kazi ya ualimu ambazo ni pamoja na kumlea mtoto kiakili, kimwili, kiroho na kijamii ili kuandaa taifa la watu wema, wazalendo na walioelimika.

Alisema walimu wanapaswa kuzisoma na kuzingatia sheria, kanuni na miongozo inayohusu utumishi wa walimu ili kuhakikisha wanafikia malengo ya serikali katika kuboresha sekta ya elimu.

Kaimu Katibu wa TSC Wilaya ya Same, John Limu alisema, nidhamu kwa walimu wilayani hapo ni nzuri kwa kuwa elimu inatolewa mara kwa mara kuhusu miiko na maadili ya utendaji wa kazi ya ualimu.

“Ndugu Mkurugenzi, hali ya nidhamu kwa walimu wa wilaya hii ni nzuri, katika kipindi cha miezi sita ni shauri moja tu la nidhamu lililofunguliwa. Ukiangalia hata kiwango cha ufaulu wa wanafunzi kwa wilaya hii ni kizuri.

Hii ni kwa sababu walimu wetu wanajitahidi kufanya kazi kwa nidhamu na weledi,” alisema Limu. Hivi karibuni Katibu MKuu wa Chama cha Walimu (CWT), Deus Seif, aliwataka walimu wajiunge na Benki ya Walimu Tanzania (MCB) ambayo licha ya kupata mikopo, watakuwa wanahisa na hatimaye ikipata faida watapata gawio.

“Tusimamie na benki yetu... Turudi kwenye benki yetu huko mikopo ipo kwa riba nafuu,” alisema Seifu wakati akizungumza na vyombo vya habari jijini Dodoma.

Aliwataka pia walimu kuacha utamaduni wa kupitisha fedha zao katika benki nyingine kwani tayari wana benki yao itakayowasaidia kupata gawio tofauti na mahali pengine

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amesema serikali imeweza ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Maalum

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi