loader
Serikali: Hospitali kujengwa kila kona

Serikali: Hospitali kujengwa kila kona

Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, David Silinde amesema kuwa Serikali inatambua uhitaji wa ujenzi wa vituo vya afya nchini ni mwingi hivyo inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo hivyo.


Silinde amesema hayo leo bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu Swali la Mbunge wa Viti Maalum (CCM), Jacqueline Msongozi lilihoji Serikali ina mpango gani wa kukarabati vituo vya afya vilivyopo wilayani Tunduru.


“Serikali imeendelea kuboresha vituo vya afya nchini ikiwemo wilayani ya Tunduru katika kipindi cha kuanzia mwaka 2017-2020 serikali imeendelea kujenga na kukarabati vituo vinne vya afya  vya Mkasale, Matemanga, Mchoteka na Nakapanya wilayani humo kwa gharama ya shilingi bilioni 1.5” amesema Silinde


Aidha, Silinde amesema kuwa kwa mwaka wa fedha 2020-2021 tayari Serikali imetenga fedha kiasi cha shilingi milioni 200 kwa ajili ya kukamilisha maboma manne ya vituo vya afya vilivyopo wilayani humo.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/4806020c5fb16d1199781bda3c9dbe28.jpg

WAFANYAKAZI wa Kituo cha Redio ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi