loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Maeneo ya Jeshi ni ya kimkakati- Serikali

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Elias Kandikwa amesema kuwa maeneo yanayomilikiwa na jeshi yamepangwa kimkakati ili kuhakikisha shughuli za jeshi zinafanyika vizuri kwa manufaa ya nchi na wananchi kwa ujumla.

Kandikwa amebainisha hayo leo bungeni jijini Dodoma alipokuwa anajibu swali la nyongeza la Mbunge wa Tarime Mjini, Michael Kembaki lililotaka kufahamu je Serikali haioni umuhimu wa kuwaruhusu wananchi wa mtaa wa Kinyambi na Bugosi katika Halmashauri ya Mji wa Tarime kufanya shughuli za kiuchumi katika maeneo yao yaliyochukuliwa na jeshi ambapo toka mwaka 2013 tathimini ya kwa ajili ya kuwalipa fidia inafanywa.

Amesema wananchi wa mitaa hiyo wanatakiwa kuvuta subira kipindi hiki Serikali inapoendelea kufanya tathimini kwa ajili ya kuwalipa fidia kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za nchi ili kuepusha mgongano katika maeneo hayo ya kimkakati.

“Mara kadhaa tumekuwa tunazungumza na muheshimiwa mbunge ili tuweze kuona kitu cha kufanya lakini kikubwa nachoweza kusema hapa ni kuwa sisi tumejipanga vizuri kuhakikisha zoezi hili la kufanya tathimini linakamilika mapema na wananchi waweze kupata haki zao” amesema Kandikwa.

WAZIRI wa Maji, Jumaa Aweso amesema serikali imeweza ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi