loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

SGR kuanza majaribio Agosti

SERIKALI  imelitaka Shirika la Reli Tanzania (TRC) kuhakikisha linatoa huduma bora na za viwango kwa Watanzania mara baada ya mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR sehemu ya Dar es Salaam hadi Morogoro kukamilika.

Mradi huo utanatarajiwa kukamilika  na kuanza kutoa huduma mwishoni mwa mwezi Agosti mwaka huu.

Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi,  Mwita Waitara, akiwatoa wasiwasi wananchi kuhusu  masuala ya miundombinu ya
umeme wa reli hiyo.

Alisema  Serikali kupitia Shirika hilo imejidhatiti kwa kuweka vyanzo vya umeme vitatu tofuati na vichwa vya kutumia dizeli ili kutatua changamoto zozote
zitakazojitokeza.

“Napenda kuwatoa wasiwasi Watanzania kuwa Serikali kupitia TRC imejipanga sawasawa kuhakikisha umeme hautakuwa na  changamoto wakati wa uendeshaji wa treni hii” amesisitiza Waitara.

Aidha, Waitara amelitaka Shirika hilo kujipanga na kuhakikisha kuwa wataalam wazawa waliopata ujuzi kwenye mradi huo wanatumika ipasavyo mara baada ya mradi kukamilika.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Masanja Kadogosa, amesema TRC imeshaajiri wahandisi zaidi ya 200 ambao kwa sasa wamewekwa kwenye miradi ili kupata ujuzi na uendeshaji wa reli hiyo ya kisasa mradi utakapokamilika.

Kuhusu upatikanaji wa mabehewa Kadogosa amefafanua kuwa tayari manunuzi yako kwenye hatua nzuri na vichwa vitawasili mapema mwezi Julai na majaribio ya treni ya kwanza kwa sehemu ya Dar es Salaam hadi Morogoro yatafanyika mwezi Agosti

SERIKALI imezuia ndege zote zinazofanya safari za kwenda ...

foto
Mwandishi: Mwandishi Wetu

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi