loader
Dstv Habarileo  Mobile
Serikali yakamilisha ununuzi wa ndege mbili mpya

Serikali yakamilisha ununuzi wa ndege mbili mpya

Serikali imesema imekamilisha  malipo  ya ununuzi  wa  ndege mpya tatu, mbili zikiwa ni Airbus A220-300 na moja ni Dash 8-Q400De-Havilland na hivyo Serikali kuwa na jumla ya ndege 12.

Akiwasilisha mwelekeo wa kazi za Serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2021/22, leo bungeni jijini Dodoma, Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amesema ndege hizo zitawasili kati ya mwaka 2021 au 2022.

“Nitumie fursa hii kulipongeza Shirika la Ndege Tanzania kwa kuanzisha safari za  kwenda Guangzhou, China,” amesema Majaliwa akibainisha kuwa safari hizo zitakuwa chachu ya kuimarisha biashara, utalii na ajira.

foto
Mwandishi: Rahimu Fadhili

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi