loader
Wabunge wataka ajenda ya taifa

Wabunge wataka ajenda ya taifa

MBUNGE wa Kawe, Askofu Josephat Gwajima (CCM) ameishauri serikali iwe na ajenda ya pamoja ya taifa ya miaka 50 kwa ajili ya maendeleo ya nchi itayozingatiwa na Rais yeyote anayeingia madarakani.

Aidha, Mbunge wa Mtama, Nape Nnauye (CCM) amewaomba wabunge wampe fursa Rais Samia Suluhu Hassan afanye maboresho ambayo yamekuwa yakifanywa hata na marais waliomtangulia.

Wameyasema hayo bungeni Dodoma wakati wakichangia bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2021/2022 iliyowasilishwa bungeni wiki hii.

Askofu Gwajima alisema ajenda ya kitaifa ni muhimu kwa kuwa kiongozi yeyote atakayechaguliwa kuongoza atatakiwa kuitekeleza.

Alisema ajenda hiyo si lazima ilingane na ya Marekani au Ulaya kwa kujenga maghorofa, ila inaweza kuwa ya kufikisha maji kwa wananchi au kusoma hadi chuo kikuu au kufanya biashara kwa uhuru.

Askofu Gwajima alisema kila kiongozi atatakiwa kuitafsiri ajenda hiyo kwa mtindo wake, kwa namna yake, kwa mikakati yake, nguvu zake au mtindo mwingine, na kinachotakiwa ni kuzingatia Katiba.

Alisema ajenda hiyo ni muhimu kwa kuwa Rais anapoingia madarakani anaweza kuamua kutotekeleza Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) au mpango wowote, na hakuna atakayemhoji kama hatoitekeleza.

Alisema kwa kuwa na ajenda hiyo, chama chochote kitakachoingia madarakani kitalazimika kuitekeleza.

Alisema hivi sasa hakuna mwendelezo kutoka utawala mmoja hadi mwingine, hivyo ni vigumu kupata maendeleo ya kutosha kwani kila kiongozi anakuja na mkazo wa jambo lake.

Alitoa mfano kuwa Serikali ya Mwalimu Julius Nyerere iliweka mkazo na kuanzisha viwanda 411 vilifanya kazi, lakini alipoingia madarakani Mzee Ali Hassan Mwinyi viwanda hakuvipa kipaumbele.

Alisema alipoingia madarakani Rais Benjamin Mkapa alibinafsisha viwanda na hata Rais mstaafu Jakaya Kikwete alipoingia madarakani hakushughulika na viwanda na alijikita kujenga miundombinu.

Askofu Gwajima alisema alipoingia madarakani Rais John Magufuli alikuja na ajenda ya Tanzania ya viwanda. Kwa upande wake, Nape aliwaomba wabunge kumwacha Rais Samia afanye maboresho kama walivyofanya marais waliomtangulia.

Nape alimnukuu Rais mstaafu Mwinyi aliyesema kwamba, ‘Kila zama kina kitabu chake.’ na kwamba Tanzania ina vitabu vitano na sasa ni kitabu cha sita, hivyo wabunge na wana- CCM wamsaidie Rais Samia aandike kitabu cha sita.

“Samia pamoja na kuendeleza ndoto nzuri za Magufuli atafanya maboresho. Hakuna mtu anasema mazuri ya JPM yanatakiwa kuachwa, isipokuwa Rais atafanya maboresho yake, aachwe kufanya hivyo,” alisema Nape.

Nape alisema amefanya kazi katika maktaba na nyaraka za CCM, miongoni mwa nyaraka moja inasema, kujikosoa na kukosolewa ni silaha ya kujenga mapinduzi ya kweli katika nchi hiyo

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/ef63f792f5c6cde018f9c5e706212182.jpg

MWENGE wa Uhuru unaendelea ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Dodoma

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi