loader
UDSM yakabidhi makumbusho Kilwa Kisiwani

UDSM yakabidhi makumbusho Kilwa Kisiwani

MKUU wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi amekipongeza Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) kwa kufanya utafiti na kuanzisha makumbusho ya malikale ya Mji Mkongwe wa Kilwa Kisiwani wilayani Kilwa yatakayowavutia wageni wengi wa ndani na nje ya nchi.

Uwekaji wa makumbusho katika mji mkongwe wa Kilwa Kisiwani ulioanzishwa kipindi cha karne ya 14 ni mwendelezo wa jitihada zilizoanza zaidi ya miaka

600 iliyopita na wenyeji wa Kilwa Kisiwani walifanya jitihada mbalimbali kutunza na kuhifadhi historia ya mji wao .

Mkuu huyo wa mkoa alitoa pongezi hizo kupitia hotuba yake iliyosomwa na Katibu Tawala wa mkoa huo, Rehema Madenge hivi karibuni kwenye halfa ya makabidhiano ya makumbusho hayo kutoka kwa Chuo Kikuu hicho na kwenda Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania (TAWA).

Alisema Makumbusho yaliyozinduliwa na kukabidhiwa kwa Tawa ni ya kwanza na ya kipekee kwa mkoa wa Lindi ,kwani yata-

vutia wageni kutoka ndani na nje ya nchi na yataongeza idadi ya watalii na mapato ya serikali yatokanayo na utalii.

“Makumbusho haya yataingiza mapato kwa Taifa letu na vile vile ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya kuongeza idadi ya watalii na kuongeza mapato yatokanayo na utalii,” alisema Zambi.

Aliongeza kuwa, “ naomba UDSM muendelee kufanya utafiti na kuja na mradi mingi ya kuendeleza Mji Mkongwe wa Kilwa na mkoa kwa ujumla ili uweze kuwa mji wa kibiashara kama iliyovyokuwa zamani kipindi cha karne ya 14.”

Zambi aliipongeza Tawa kwa juhudi kubwa ya kutunza na kuendeleza malikale ya Kilwa na kutunza magofu ya kale ambayo yapo hatarini kutoweka kutokana na mabadiliko ya tabianchi .

Alisema serikali ya mkoa huo itaendelea kushirikiana na Tawa, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na taasisi nyingine mbalimbali ili kuleta miradi mbalimbali itakayowezesha kukuza utalii ndani ya mkoa huo wenye historia kubwa ya kuwa na malikale.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Tawa ,Meja Jenerali Mstaafu Hamisi Semfuko alisema utalii wa Tanzania Bara kwa miaka

mingi umekuwa ni wa wanyamapori, lakini sehemu ambayo yenye kuweza kuvutia watalii wengi zaidi wa ndani na nje ya nchi ni wa utalii wa malikale , fukwe ,magofu na viumbe vya chini ya bahari.

Alisema Tawa kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wamefanikisha kuona azimio la Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Damas Ndumbaro kuhusu kufufua na kuendeleza utalii wa malikale unafanyika kwa kuanzia na Kilwa .

Kwa upande wake Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa William Anangisye alisema kuwekwa kwa makum-

busho ya Kilwa Kisiwani ni zao la kuibuka kwa ugonjwa wa Korona.

Alisema kuibuka kwa ugonjwa huo kulisababisha watafiti washiriki kutoka nje ya nchi kushindwa kuja Tanzania ili kuungana na wenzao kutoka Idara ya Mambo ya Kale , Makumbusho ya Taifa na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Profesa Anangisye alisema kuweka makumbusho Kilwa Kisiwani yenye vioneshwa haikuwa mojawapo ya malengo ya kutekeleza mradi wa ufafiti ambao kwa pamoja unafadhiliwa na Chuo Kikuu hicho na Chuo Kikuu cha St Andrews cha nchini Uingereza.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/78a5c238183f204d8db6fe8f26517469.jpeg

WAFANYABISHARA mbalimbali wa Temeke, ...

foto
Mwandishi: John Nditi, aliyekuwa Kilwa

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi