loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Migne: Harambee ilikuwa dhaifu

KOCHA wa zamani wa timu ya taifa ya Kenya, Harambee Stars, Sebastian Migne amesema aliichukua timu hiyo ikiwa dhaifu wakati wa kipindi chake cha kuifundisha.

Mfaransa huyo amesema hayo  katika barua yake wakati akiomba nafasi ya kufundisha timu ya taifa ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Migne ambaye aliwahi kuifundisha timu ya taifa ya Guinea ya Ikweta, pia alifurahia maisha akiwa na klabu ya daraja la pili ya Ufaransa ya Chamois Niortais FC  aliyodumu nayo kwa muda mfupi tangu alipoondoka Kenya na sasa anataka kumbadili Christian Biembe katika kikosi cha Chui kwa ajili ya kufuzu kwa Kombe la Dunia 2022.

 

“Napenda kuwahakikishia nyinyi kuwa nitawasaidia kuiwezesha timu yenu kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia 2022 baada ya mechi za raundi ya pili ambayo inaanza Juni itakayomalizika kwa mechi za mchujo katka tarehe za Fifa baadae Novemba.”

“Mimi ni kocha wa timu za taifa mwenye uzoefu mkubwa Afrika, hasa Congo kama kocha msaidizi kuanzia mwaka 2011 hadi 2013. Naijua vizuri sehemu hiyo. Nimekuwa na matokeo mazuri kila mahali, wakati mwingine timu ya taifa (wakati nikiwa kazini) ilikuwa dhaifu,” alisema.

Migne alikuwa akiifundisha timu ya taifa ya Kenya kati ya mwaka 2018 na 2019.

 

Wakati wa kipindi chake, aliisaidia Harambee Stars kufuzu kwa fainali za Mataifa ya Afrika, Afcon kwa mara ya kwanza kwa zaidi ya miaka 10 mwaka 2019, huku timu hiyo ikizishinda Ghana na Ethiopia jijini Nairobi.

 

Pia alishuhudia ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa huko Madrid kabla ya kuachia nafasi hiyo baada ya kufungwa na Tanzania, Taifa Stars mwaka 2020 katika mechi za kufuzu kwa michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa nyumbani (Chan).

 

Migne ambaye alitengeneza jina wakati akiwa msaidizi wa kocha Mfaransa, Claude Le Roy wakati wa historia yake ya kufundisha soka, aliahidi kutenda haki wakati wa jukumu lake katika DRC.

 

“Nataka kufanya kazi na wachezaji wenye nidhamu, wakiwa pia na ari kubwa na wenye kujituma na wachezaji bora wa ndani wenye uwezo mkubwa,” alisema.

 

Migne pia alikuwa akihusishwa na nafasi ya kufundisha vigogo wa soka wa Tanzania, Yanga ambayo hadi saa iko chini ya kocha wa muda Juma Mwambusi.

 

DRC imepangwa pamoja na Benin, Madagascar na Tanzania katika mbio za kusaka nafasi ya kufuzu kwa fainali za Kombe la Dunia Qatar wakati Kenya itakuwa na kibarua dhidi ya Mali, Uganda, na Rwanda.

 

KOCHA wa Simba, Didier Gomes na wa Yanga, ...

foto
Mwandishi: NAIROBI, Kenya

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi