loader
Dstv Habarileo  Mobile
Kipchoge ataka dhahabu nyingine Olimpiki

Kipchoge ataka dhahabu nyingine Olimpiki

MWANARIADHA anayeshikilia rekodi ya dunia ya marathoni kwa wanaume, Eliud Kipchoge amesema kwa sasa ameelekeza nguvu zake ili kutwaa medali ya pili ya dhahabu ya Olimpiki baada ya kushinda mbio huko Enschede, Uholanzi.

Kipchoge alikuwa akishindana kwa mara ya kwanza baada ya kumaliza katika nafasi ya nane London Marathoni Oktoba mwaka jana.

"Haya yalikuwa majaribio ya kweli ni maandalizi kuelekea Michezo ya Olimpiki.  Ukizingatia sasa tunaangalia Olmpiki. Nitawasiliana na kocha wangu na benchi la ufundi kuangalia nini kijacho kwa ajili ya maandalizi ya Tokyo," alisema Kipchoge.

Bingwa huyo wa Olimpiki alimaliza marathoni hiyo juzi kwa kutumia saa 2:04:30 akiwa wa kwanza mbele ya mshirika wake katika mazoezi, Jonathan Korir aliyemaliza wa pili kwa 2:06:40, huku Eritrean Goitom Kifle alikuwa watatu kwa saa 2:08:00.

Kipchoge alisema anahisi kujiamini zaidi kufuatia ushindi huo baada ya matatizo ya sikio na nyama za paja na matatizo mengine yaliyomnyima ushindi wa tatu wa London Marathoni mwaka jana, ambako Muethiopia Hura Kitata alimaliza wa kwanza.

Kipchoge ni sehemu ya watu wanne waliochaguliwa na Riadha Kenya kuongoza nchi yao kusaka medali katika Michezo ya Olimpiki.

Wengine katika timu hiyo ni pamoja na bingwa wa Boston Marathoni Lawrence Cherono, Vincent Kipchumba na bingwa wa medali ya tatu ya dunia, Amos Kipruto.

Katika mbio za wanawake, Mjerumani Katharina Steinruck alimaliza wa kwanza kwa kutumia saa 2:25:59  mbele ya Mreno Sara Moreira (2:26:42) na mwenzake wa nchi hiyo, Rabea Schoneborn (2:27:03) waliomaliza wa pili na tatu.

Mkenya Gladys Chesir alimaliza wa nane kwa kutumia saa 2:29:16.

https://apps.tsn.go.tz/public/uploads/ca1ad6d5b9793ed2460e989ba866de28.jpg

BAADA ya Yanga kuondolewa kwenye michuano ya Ligi ...

foto
Mwandishi: NAIROBI

Post your comments

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi