loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Drogba amfariji Mourinho

Mshambuliaji wa zamani Chelsea na mfungaji bora wa muda wote wa Timu ya Taifa ya Ivory Coast, Didier Drogba, kupitia mtandao wa Instagram amemuambia Kocha wa zamani wa Tottenham Jose Mourinho “furahia maisha yako” baada ya kutimuliwa na klabu hiyo.

Mourinho amefukuzwa zikiwa zimesalia siku sita kabla ya kuwakabili Manchester City kwenye mechi ya fainali ya Kombe la Carabao, itakayopigwa Jumapili hii.

Drogba ambaye alifurahia makombe kwa miaka mingi akiwa na Mourinho kama kocha wake, aliandika ujumbe ‘Enjoy your life ze,’ (furahia maisha yako) huku akiambatanisha na vikatuni vikatuni vya kucheka ‘laughing emojis’.

Ni wazi kuwa mashabiki wengi wa Tottenham wanashauku ya kujua ni nani atachukua nafasi ya ukocha klabuni hapo baada ya Mourinho.

MANCHESTER United leo itaikaribisha Liverpool katika ...

foto
Mwandishi: Mitandao

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi