loader
Dstv Habarileo  Mobile
Picha

Uharibifu wa mazingira wakausha maji

MJI wa Mpwapwa pamoja na viunga vyake mkoani Dodoma, unakabiliwa na uhaba wa maji kutokana na uharibifu mkubwa mazingira  unaoendelea kufanyika katika vyanzo maji vinavyosambaza maji katika mji huo.

Hali hiyo imebainishwa na Timu ya Watalaamu wa Mamlaka ya Maji wilayani Mpwapwa waliotembelea vyanzo vya Mayawile kuona hali halisi ya uharibifu  unaofanywa na shughuli za kibinadamu katika vyanzo hivyo.

Meneja wa Mamlaka ya Maji na Safi na Usafi wa Mazingira (MPWAUSA) Peter Kabelwa alisema kwa sasa  vyanzo vyote vya asili viko mbioni kukakuka kutokana na uharibifu mkubwa wa mazingira  katika vyanzo vya maji vinavyo hudumia zaidi ya wakazi 29,429.

 

Aidha Kabelwa alisema kwa wakazi wa Mpwapwa wapatao 46,429 ambao wanahudumiwa na vyanzo vya Mayawile ni zaidi ya wakazi  29,429, wapo katika hatari ya kukosa maji kabisa kutokana na vyanzo vya maji kukaribika kukauka.

 

Aidha alisema pia mji huo kwa sasa unategemea maji yanayopatikiana

katika mradi wa maji ya kisima cha Kikombo, ujulikanao kama mradi wa

mkenya uliojengwa zaidi ya miaka 10 iliyopita ambao nao kutokana na

mvua za mwaka jana na mwaka huu kunyesha kwa wingi, zimeharibu

miundombinu na baadhi ya mabomba kusombwa’’.

Kabelwa alisema, mkakati uliopo ni kuimarisha huduma hizo kwa kufanya

ukarabati wa miundombinu iliyoharibika na  kuomba fedha wizarani ili

kuweza kuchimba visima vingine ambayo vitasaidiana na kisima cha

Kikombo.

Mmoja wa wakazi wa mji wa Mpwapwa,  Maria  Selemani alisema, kwa sasa huduma za maji  katika mji wa Mpwapwa zimekuwa hafifu sana kitu

alichosema kinasababisha hali ya maisha kupanda.

Alisema kwa sasa wanachota maji kwa mgao siku zingine hadi siku mbili

zinapita bila maji kutoka bombani.

Meneja wa Ufundi wa Mamlaka hiyo, Winner Noel alikiri tatizo hilo

kuwapo  ambalo alisema changamoto hiyo imesababishwa na  miundo mbinu mingi kusomwa na maji na wateja walikuwa wanatumia vyanzo vya

mtiririko  kuharibu  vyanzo vya maji ambavyo vinatishia kukauka.

SERIKALI imezuia ndege zote zinazofanya safari za kwenda ...

foto
Mwandishi: Magnus Mahenge, Mpwapwa

Post your comments

Tangazo

CRDB

Habari Nyingine

Categories

habari zaidi zinazoendana na hii

mpya # zaidi